• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 1:05 PM
Wanafunzi wa kike kunufaika na ufadhili wa sodo

Wanafunzi wa kike kunufaika na ufadhili wa sodo

Na LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya matunda ya Delmonte Kenya Limited (DMKL), ya Thika, imeanza mpango wa kusambaza sodo kwa wasichana ambao ni wanafunzi wa shule za msingi na za upili.

Meneja wa masoko na mauzo wa kampuni hiyo Bi Margaret Nyoro, alisema kampuni hiyo itaendesha mpango huo kwa miezi mitano mfululizo kuanzia mwezi Juni 2021.

Akisema watasambaza paketi 5,200 za sodo kwa wanafunzi wapatao 900 kwa muda huo.

“Mpango huo ni muhimu sana kwa wanafunzi hao kwa sababu wataweza kuendelea na masomo yao bila shida. Hata wazazi wamefurahia hatua hiyo,” akasema Bi Nyoro.

Alieleza wanafunzi hao wanatoka katika shule za msingi za Kihunguro, na Ndula. Halafu za upili ni ya Delmonte Mixed Secondary, na Ndula secondary.

Alieleza kuwa kampuni ya Sunday International itasambaza sodo 2,310 nayo kampuni ya African Cotton Industry ya Flora Sanitary Pads, itasambaza 2,000.

Baadhi ya wanafunzi watakaonufaika na mpango huo ni wale wanaotarajia kufanya mtihani wao wa 2021.

“Tunajua wazazi wengi hulemewa kuwanunulia mabinti zao bidhaa hiyo hivyo tumeonelea ni vyema kuingilia kati kama kampuni,” alisema Bi Nyoro.

Alieleza kampuni ya Delmonte kwa ushirikiano na wakfu wa United Nations Foundation (UNF), watawahamasisha wanawake wapatao 10,000 waelewe vyema maswala ya kiafya ili nao wakienda mashinani wawe na ufahamu wa kuwasaidia wasichana kuhusu maswala ya kiafya.

Alisema utafiti uliofanywa majuzi umebainisha kuwa asilimia 65 ya wanawake na wasichana nchini hawana uwezo wa kununua sodo kila mwezi.

Pia imebainika kuwa wasichana wengi hukosa kuhudhuria masomo iwapo hawana sodo.

“Tumegundua ya kwamba wanafunzi wasichana wa Darasa la Sita na Darasa la Nane hukosa kuhudhuria masomo wanapokosa sodo za kujikimu,” alieleza meneja huyo.

Akisema muda wa wiki 144 hupotea bure bila wanafunzi hao kuhudhuria masomo.

You can share this post!

Vuguvugu la Linda Katiba halitachoka kunusuru nchi – Karua

Bunge la Vihiga kujadili iwapo mawaziri wanne watimuliwe au...