• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Familia yaomba isaidiwe kutafuta mwili wa jamaa aliyezama Mto Sabaki

Familia yaomba isaidiwe kutafuta mwili wa jamaa aliyezama Mto Sabaki

NA ALEX KALAMA

Familia moja katika eneo la Marereni eneo bunge la Magarini kKaunti ya Kilifi inaomba serikali na wahisani kujitokeza na kuwasaidia kuupata mwili wa mpendwa wao aliyezama maji boti alilokuwa akisafiria lilipozama katika Mto Sabaki.

Naibu Kamishina wa eneo Bunge la Magarini, Bw Peter Thiongo alithibitisha kisa hicho.

“Kwa sasa ile ripoti ambayo imenifikia ni ya yule kijana ambaye aliaga baada ya boti kuzama katika Mto Sabaki. Lakini bado tunaendelea kufuatilia ili tujue iwapo kunao wengine waliopoteza maisha,” alisema Bw Thiongo.

Kulingana na baba ya kijana huyo John Chea, kisa hicho kilitokea juma moja lililopita wakati kijana huyo alipokuwa akivuka mto huo kuelekea Malindi ili kufanya biashara yake ya kuuza makaa.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Marereni, Bw Chea alisema kuwa licha ya juhudi za familia hiyo kuutafuta mwili wa jamaa yao siku kumi zilizopita, bado hawajafanikiwa.

“Nimepoteza mtoto wangu katika Mto Sabaki nimetafuta kwa muda wote hatujamuona, naomba kama kuna usaidizi wowote kutoka kwa serikali au wahisani watusaidie,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Msaada hatimaye wawasili Lamu kunusuru wakazi wanaozongwa...

Maisha ya wanaume yanaendelea kuwa mafupi tangu mlipuko wa...

T L