• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Maisha ya wanaume yanaendelea kuwa mafupi tangu mlipuko wa corona, watafiti wamebaini

Maisha ya wanaume yanaendelea kuwa mafupi tangu mlipuko wa corona, watafiti wamebaini

Na CECIL ODONGO

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Carlifornia Marekani wamebaini kuwa mwanya kati ya maisha ya mwanaume na mwanamke unaendelea kupanuka tangu janga hilo lililoanza mnamo 2019. Huku muda wa uhai wa wanaume ukiendelea kupungua, ule ya wanawake hauna mabadiliko yoyote.

Kando na janga la corona, visa vya kujitia kitanzi, matumizi ya dawa za kulevya, ajali miongoni mwa matukio mengine, yamekuwa yakiwaathiri wanaume mno ikilinganishwa na wanawake.

“Kupungua kwa muda wa uhai wa wanaume kumechangiwa na kujitia kitanzi, uraibu wa kutumia dawa za kulevya unaoishia magonjwa kama ya ini. Wanaume wengi pia ndio huangukiwa sana na mzigo wa uchumi na huishia kuandamwa na msongo wa mawazo,” ikasema utafiti huo.

“Japo vifo kutokana na mihadarati vimeongezeka miongoni mwa wanaume na wanawake, ni wazi kuwa wanaume ndio wengi ukitathmini takwimu za mauti haya,” ikaongeza utafiti huo.

Kabla ya ujio wa virusi vya corona, visababishi vikuu vya mauti kwa wanaume vilikuwa kujitia kitanzi, magonjwa ya moyo, mauaji kutokana na mizozo ya kinyumbani, ajali na ugonjwa wa sukari.

Mwanzo wakati wa corona, hatua ya wanaume wengi kuchelea kusaka matibabu, kuwa kwenye hatari zaidi ya maambukizi, matatizo ya kiakili, mizozo ya nyumbani pia iliwaathiri wanaume na kusababisha mauti yao.

Tangu wakati huo hakujakuwa na mabadiliko sana kwa sababu baadhi ya wanaume ambao walipoteza ajira bado hawajarejea kazini. Isitoshe mzigo wa kiuchumi unaendelea kuwa kubwa na kutikisa wanaume, ambao ndio wanategemewa sana katika familia nyingi.

Kuyaokoa maisha ya wanaume na kuwawezesha kuishi kwa kipindi kirefu, watafiti hao wanapendekeza kuwa, juhudi kubwa zinastahili kuwekezwa katika kutoa ushauri kwa wanaume hasa kuhusu afya yao ya kiakili.

  • Tags

You can share this post!

Familia yaomba isaidiwe kutafuta mwili wa jamaa aliyezama...

Jombi pabaya kwa kudai mvua ya mafuriko ni adhabu ya Mungu

T L