• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Familia yaomba msaada kurejesha maiti ya jamaa yao hapa nchini kutoka UJerumani, wakihofia utachomwa

Familia yaomba msaada kurejesha maiti ya jamaa yao hapa nchini kutoka UJerumani, wakihofia utachomwa

NA FARHIYA HUSSEIN

FAMILIA moja kutoka eneo la Pwani imeomba Wizara ya Mashauri ya Kigeni kuingilia kati na kuwasaidia kuurudisha mwili wa jamaa yao nchini kutoka Ujerumani kabla haujateketezwa.

Bi Mwanaharusi Nihazi aliyefariki Novemba 9, 2023 ameishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 30.

Kulingana na kakake Nihazi, Bw Mohamed Rama Kadunge, mwendazake alikuwa akiugua kansa ya mapafu.

Familia hiyo sasa inatakiwa kuwa na Sh300, 000 ili kulipa bili za hospitali na kusafirisha mwili wa jamaa yao kurudi nchini kwa minajili ya mazishi.

“Tumefanikiwa kupata Sh75, 000 kufikia sasa. Dadangu ndiye alikuwa mlezi wa familia hii. Alinipeleka shuleni mpaka sasa nimekuwa mtu mzima. Tulikuwa katika harakati ya kupanga safari yangu ya kuenda kufanya kazi Ujerumani,” alisema Bw Kadunge huku akibubujikwa na machozi.

Bi Nihazi aliishi peke yake Ujerumani kufuatia kifo cha mumewe mwaka wa 2007.

Familia hiyo imeiandikia barua Wizara ya Mashauri ya Kigeni kupitia shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Africa wakiomba msaada ili mwili wa Bi Nihazi urudishwe nchini.

“Wajerumani wanasema tusipotoa mwili huko kwa wakati utachomwa. Tunaomba usaidizi ili azikwe kwa heshima kulingana na mila,” alisema Bw Kadunge.

 

 

  • Tags

You can share this post!

Mke wa Trossard alia mumewe kuadimika chumbani

El-Nino yalemea Pwani maafa yakishuhudiwa

T L