• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Gavana wa Nyamira motoni kwa kumfuta kazi Waziri wa Afya

Gavana wa Nyamira motoni kwa kumfuta kazi Waziri wa Afya

Na RUTH MBULA

UAMUZI wa Gavana wa Nyamira, Amos Nyaribo kumfuta kazi Waziri wake wa Afya, Dkt Timothy Ombati, kwa madai ya ufisadi, umekashifiwa na baadhi ya wawakilishi wa wadi wa kaunti hiyo.

Wawakilishi hao wanataka gavana kujiuzulu, wakisema waziri alifutwa kwa njia isiyo ya kawaida.

Bw Nyaribo alimfuta kazi Dkt Ombati kwa madai kuwa waziri huyo wa afya alifuja takriban Sh37 milioni zilizokusudiwa kununua dawa za hospitali mbalimbali za kaunti hiyo, ikiwa ni pamoja na hospitali ya Nyamira Level Four.

Gavana huyo alipatia waziri barua ya kufutwa kazi wiki jana baada ya kumalizika kwa likizo ya lazima ya siku 30.

Bw Nyaribo alimlaumu Dkt Ombati kwa kupotosha afisi ya gavana kuhusu ununuzi wa dawa za thamani ya Sh37milioni za hospitali za kaunti hiyo.

Hata hivyo, wawakilishi wa wadi wakiongozwa na Naibu Spika, Thaddeus Nyabaro na Naibu Kiongozi wa Wengi, Duke Masira waliungana na viongozi wa eneo hilo kulaani gavana Nyaribo kwa kumfuta kazi Dkt Ombati.

Walidai waziri alikuwa akionewa kwa sababu si wa ukoo wa gavana.

Kadhalika, walimtaka gavana huyo kujiuzulu la sivyo ashtakiwe kwa kile walichodai kuwa ni matumizi mabaya ya mamlaka.

“Ili haki itendeke, Bw Nyaribo anafaa kuondoka ofisini ili kuruhusu uchunguzi ufanywe kubaini ukweli kuhusu madai ya wizi wa pesa zilizotumika kwa ununuzi wa dawa katika hospitali za umma,” Bw Nyabaro akasema.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa waimarisha msako dhidi ya Al-Shabaab baada ya gari...

Matumaini kwa wakulima serikali ikiahidi kulipa fidia baada...

T L