• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 3:24 PM
Hospitali ya Tigoni yatoa hewa ya oksijeni bure kwa wagonjwa

Hospitali ya Tigoni yatoa hewa ya oksijeni bure kwa wagonjwa

Na LAWRENCE ONGARO

KAUNTI ya Kiambu inaendelea kuwapa wagonjwa wa Covid-19 oksijeni ya bure huku walioathirika wakifurika katika hospitali ya Tigoni.

Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro alisema mmiliki wa kiwanda cha Devki Steel Mills, mjini Ruiru Bw Navendra Raval ‘Guru’, amefungua eneo la kujaza mitungi na hewa ya oksijeni, huku akisambaza kwa hospitali kadha bila malipo.

Masharti ya ‘Guru’ ni kwamba hospitali hizo zitumie hewa hiyo ya oksijeni kuwafaa wagonjwa bila ya kuwatoza ada.

Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo ili kuwasaidia wagonjwa wengi ambao wamelemewa kulipa malimbikizo ya bili ya matibabu hasa hewa ya oksijeni.

Baada ya Kaunti ya Kiambu kuhifadhi hewa hiyo katika mitungi maalum wagonjwa wengi kwa sasa wanafurika katika hospitali ya Tigoni wakitafuta matibabu ya dharura ya homa ya Covid-19.

Hospitali ya Tigoni imeweka mitungi ya hewa ya oksijeni ya uzito wa tani tatu ambayo hujazwa baada ya muda wa saa 48.

Gavana Nyoro alisema tayari hospitali hiyo ina vitanda 250, akiongeza kuwa wagonjwa wengi wametoka kaunti jirani kutafuta matibabu.

Baadhi ya wagonjwa hao wanatoka kaunti za Nairobi, Kajiado, Nakuru, na Murang’a.

You can share this post!

Chelsea wapiga West Ham United na kuingia ndani ya nne-bora...

Olunga akwamilia juu ya jedwali la wafungaji Klabu Bingwa...