• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:53 PM
Huduma ya simu kusaidia kudhibiti maradhi yasiyoambukizwa

Huduma ya simu kusaidia kudhibiti maradhi yasiyoambukizwa

NA PAULINE ONGAJI

SASA utaweza kupata vidokezo kuhusu jinsi ya kuzuia, kutambua na kudhibiti maradhi yasiyoambukizwa (NCDs).

Hii ni kupitia huduma mpya ya simu ya mkononi kwa jina Fafanuka, inayosambaza maelezo na taarifa kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa kama vile kisukari, maradhi ya moyo, kansa na kifafa kisukari.

Huduma hii ambayo ni ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, kampuni ya mawasiliano ya Safaricom PLC, Savannah Informatics, na Muungano wa mashirika yanayohusiana na maradhi yasiyosambaa nchini NCDAK, inanuiwa kutoa taarifa sahili kuhusu magonjwa haya; ishara, hatari, jinsi ya kuzuia, kutambua na kudhibiti, kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Madhumuni ya jukwaa hili ni kutoa maelezo kwa wananchi kuhusu maradhi haya, vile vile ushauri wa jinsi ya kudumisha afya njema. Huduma hiyo itagharimu Sh10 kwa kila ujumbe utakaotumwa kila wiki.

Kulingana na Wizara ya Afya, maradhi yasiyoambukizwa yanawakilisha asilimia 40 ya vifo vyote nchini, huku watu walio chini ya umri wa miaka 40 wakiwa katika hatari kubwa.

Mwaka wa 2021, takriban asilimia 39 ya vifo vilitokana na maradhi hayo, ongezeko kutoka asilimia 27 mwaka wa 2014. Inatabiriwa kwamba kufikia mwaka wa 2030, huenda vifo vinavyotokana na maradhi haya vikafikia asilimia 55.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Hatua zichukuliwe kuwaokoa Wakenya...

Mtaalam anayewashauri wagonjwa jinsi ya kutumia vifaa vya...

T L