• Nairobi
  • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
Mtaalam anayewashauri wagonjwa jinsi ya kutumia vifaa vya sauti masikioni

Mtaalam anayewashauri wagonjwa jinsi ya kutumia vifaa vya sauti masikioni

NA MAGDALENE WANJA

BI Wairimu Mwangi ni mtaalam wa maswala ya masikio na sauti (clinical audiologist), kazi ambayo amaifanya kwa muda wa miaka 10.

Anafanya kazi katika kampuni ya Starkey Hearing Technologies-Africa, ambayo inatengeneza vifaa vya kusaidia wenye matatizo ya kusikia.

“Nilipokuwa mdogo, nilitamani sana kuwa daktari, na nilipokuwa mdogo, tayari wanafamilia walizoea kuniita daktari. Kwa upande mwingine , nilipenda kuimba na nilitamani kuwa mwanamuziki,” akasema Wairimu.

Katika kampuni hiyo, kazi yake kuu ni kuwapa mafunzo wataalamu pamoja na wagonjwa jinsi ya kutumia vifaa hivyo ili kupata manufaa zaidi.

Wairimu huwafunza wagonjwa wenye changamoto za kusikia jinsi ya kutumia vifaa vipasavyo ili kuwawezesha kujitegemea.

“Pia ninawapa mafunzo wataalam jinsi ya kuwapa wagonjwa hao huduma bora, pamoja na kuelewa changamoto mbalimbali ambazo huwa wanazipitia,” alisema Wairimu.

Wairimu anasema kuwa ili kufuzu kuwa mtaalamu katika sekta hii, lazima ujiunge na chuo cha sayansi ya afya.

Mtaalam Wairimu Mwangi anayefanya kazi katika kampuni ya Starkey Hearing Technologies-Africa, ambayo inatengeneza vifaa vya kusaidia wenye matatizo ya kusikia. PICHA | MAGDALENE WANJA

Aliongeza kuwa ni muhimu kuwa na wshauri ambao wana uzoefu zaidi katika sekta unayoienzi.

“Japokuwa nilipatwa na tatizo sawa na hilo nilipokuwa mchanga, nimekuwa na nia ya kufanya vyema katika sekta hii kuwasaidia wagonjwa,” aliongeza.

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kwamba aslimia tano ya idadi ya watu duniani wako na changamoto ya kusikia. Hii ni sawa na watu 430 milioni.

Idadi hii inakadiriwa kuongezeka kufikia mwaka 2050.

  • Tags

You can share this post!

Huduma ya simu kusaidia kudhibiti maradhi yasiyoambukizwa

Mwanasaikolojia Faith Gichanga ataka kampuni, watu binafsi...

T L