• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Idadi ya watu walioangamia Shakahola yagonga 109

Idadi ya watu walioangamia Shakahola yagonga 109

NA ALEX KALAMA

MAAFISA wanaoendeleza operesheni ya kufukua makaburi ili kutoa mili ya waliokuwa waumini wa dhehebu tata la Good News International kwenye msitu wa Shakahola kimepata miili 11 hii leo Alhamisi.

Hii ni baada ya maafisa hao kufukua makaburi 10 katika shamba linalodaiwa kuwa la mhubiri tata Paul Mackenzie na kufanya idadi ya watu walioangamia kutokana na kile kimerejelewa kama imani potovu kugonga 109.

Msitu wa Shakahola. PICHA | ALEX KALAMA

Kati ya miili hiyo 11 iliyopatikana Alhamisi, miili mitano ni ya watoto huku sita ikiwa ya watu wazima.

Hata hivyo miili hiyo imesafirishwa kwenda kuhifadhiwa katika kontena la kuhifadhia miili ya wahanga wa imani potovu ambalo limeweka karibu na mochari ya wafu katika hospitali kuu ya kaunti ndogo ya Malindi. Hii ni baada ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo kujaa.

Msitu wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi. PICHA | ALEX KALAMA

Vilevile operesheni ya kufukua makaburi katika msitu wa Shakahola bado itaendelea Ijumaa huku shughuli ya upasuaji wa mili hiyo na kuifanyia uchunguzi ili kubaini kilichosababisha vifo vyao ikitarajiwa kufanyika kuanzia wiki ijayo.

  • Tags

You can share this post!

Kizaazaa Eric Omondi apeleka maandamano Kisumu

Muungano wa wachungaji Kilifi wataka wenye mahubiri potovu...

T L