• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:19 PM
Italia yapepeta Wales na kufikia rekodi ya kutoshindwa katika mechi 30 mfululizo

Italia yapepeta Wales na kufikia rekodi ya kutoshindwa katika mechi 30 mfululizo

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

WALES walitinga hatua ya 16-bora licha ya kupigwa 1-0 na Italia katika Kundi A kwenye fainali zinazoendelea za Euro.

Kikosi hicho cha kocha Robert Page kilikamilisha mechi na wachezaji 10 uwanjani baada ya Ethan Ampadu kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea Federico Bernardeschi visivyo.

Italia waliojibwaga ugani wakiwa tayari wamefuzu kwa hatua ya muondoano, walikamilisha kampeni za kundi lao kileleni baada ya kujizolea alama tisa, tano zaidi kuliko Wales na Uswisi waliowacharaza Uturuki 3-1 jijini Baku, Azerbaijan. Uturuki waliaga kipute cha Euro bila alama yoyote.

Chini ya kocha Roberto Mancini, Italia walifungiwa bao la pekee na la ushindi dhidi ya Wales kupitia kwa Matteo Pessina. Italia sasa watakutana na kikosi kitakachoambulia nafasi ya pili kwenye Kundi C linalojumuisha Uholanzi, Ukraine, Austria na Macedonia Kaskazini.

Ushindi wa Italia uliendeleza ubabe ambao sasa umewashuhudia wakikosa kupigwa katika mfululizo wa mechi 30 zilizopita kwenye mashindano yote.‘The Azzuri’ wameshinda mechi 25 kati ya hizo tangu Septemba 2018 walipocharazwa 1-0 na Ureno. Sasa wamefikia rekodi yao ya awali ya kutopigwa katika jumla ya mechi 30 mfululizo kati ya Novemba 1935 na Julai 1939.

 

  • Tags

You can share this post!

MICHEZO: Kiota ambacho kinaelekea kufikia malengo ya...

Aliyejaribu kumuua Kosewe asema alikuwa akijikinga