• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 2:55 PM
Jamii ya Sengwer yalia viongozi kusahau eneo lao kimaendeleo

Jamii ya Sengwer yalia viongozi kusahau eneo lao kimaendeleo

Na GERALD BWISA

JAMII ya Sengwer katika eneo la Makutano, eneobunge la Cherang’any, Kaunti ya Trans Nzoia, imeshutumu viongozi waliochaguliwa kwa kuibagua katika miradi ya maendeleo.

Jamii hiyo Jumatano ilisema kuwa eneo lao halina kituo cha afya na barabara zote ni mbovu.

“Tulilazimika kumbeba mwanamke mmoja aliyetaka kujifungua hadi katika kituo cha afya kilichoko mbali kwa sababu barabara zetu ni mbovu,” akasema Elija Yaraten, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Walisema barabara inayounganisha maeneo ya Makutano imekuwa katika hali mbaya baada ya kutengezwa na serikali ya Kaunti mwaka 2020.

“Tunashangaa kwa nini mwakilishi wadi wetu, Stephen Njoroge ameshindwa kutimiza ahadi yake ya kututengenezea barabara,” akasema Lina Chepkoech.

Kadhalika, wanawashutumu viongozi wao kwa kubagua katika ajira huku wakisema kuwa vijana wao wanaohitimu elimu ya vyuoni hawajaajiriwa katika serikali ya kaunti.

“Tunataka kujua ni kwanini serikali ya kaunti ya Trans Nzoia imetenga jamii yetu. Tuna haki ya kufanyiwa maendeleo na serikali ya kaunti,” akasema Bw Wycliffe Misoga, mkazi.

Bw Misoga pia alitaka wizara ya uratibu wa mambo ya ndani kuwachagua wakazi wa eneo lao katika nafasi za chifu msaidizi.

You can share this post!

Vigogo wa KNUT, KUPPET sasa waanza kuhemeshwa

Chuo chachunguza ‘wadudu’ wawe mlo