• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Jinsi wanaume wanavyolaghaiwa na wanawake ili kulea watoto ambao si wao

Jinsi wanaume wanavyolaghaiwa na wanawake ili kulea watoto ambao si wao

NA FRIDAH OKACHI

“NAMLEA mtoto wangu ambaye ana baba watatu ambao si halali,” asimulia EW (ufupisho wa jina lake). Mkazi huyu wa Kasarani, ana mtoto mmoja anayelea na baba watatu, kila baba akijukumika kwa mahitaji ya mtoto huyo bila kujua si wao.

Akiwa na umri wa miaka 21, alifanya uamuzi wa kuingia kwenye ndoa kutokana na mazingira aliyolelewa. Alihisi mama mzazi na baba wa kambo walimtenga kwa kukosa kumpa nafasi ya kusoma, nduguze watatu wakipelekwa shule za bweni na kusalia katika shule ya kutwa.

“Kupata alama ya C haikuwa rahisi kwangu pale Dandora, nilijiunga na shule ya upili kutokana na kupita mtihani wa Darasa la Nane. Tatizo lilikuwa kulipiwa karo, sikuwa naelewa kwa nini wazazi wangu hawalipi na walikuwa na uwezo,” alieleza.

Baada ya shule ya upili alifanya uamuzi wa kuingia ndoa na mumewe ambaye aligundua kuwa ana mahusiano ya nje na kumhukumu kuwa tasa.

EW mbaye ni mfanyabiashara alimfahamu mumewe kuwa na mkono mrefu na dharau. Kulingana na mfanyabiashara huyo, mume huyo alikuwa akifanya hivyo ili kumzuia kuenda kazini.

“Kila wakati nilimpata na mwanamke mwingine, aliniita tasa,” asimulia.

Dharau zilizidi na kulazimika kuondoka. Uamuzi huo ni baada ya mumewe kumfukuza wakati alimfumania na rafikiye wa kike katika chumba cha kulala.

“Kuna wakati nilifunga kazi mapema, kufika nyumbani nikapata mlango upo wazi. Kuingia kwenye chumba cha kulala, nilipata akiwa  na rafika yangu nilipotaka kufahamu zaidi, nilipokea kichapo na nguo zangu zikawekwa kwenye mabegi makubwa. Kilichoniumiza, nguo zangu za ndani ambazo zilikuwa baridi alifunga kwenye karatasi ya plastiki kinyume na imani ya jamii yangu,”alisimulia.

Baada ya juma moja alifahamu ana ujauzito ambao alihusisha wanaume watatu. Hivi sasa, kila mmoja anagharamia kwa majukumu ya mtoto.

“Nilishindwa kumweleza baba ya mtoto nina ujauzito wake, kila wakati alinihukumu na kuniita tasa,” anasimulia.

Kulingana na EW, alikataa kumfahamisha akijua kuwa iwapo atamwambia aliyekuwa mumewe, angelazimika kurudi.

“Uamuzi wangu kukosa kumwambia ni kwa sababu nilijua angetaka nirudi. Na sikuwa tayari kurudi nikikumbuka aliyonifanyia,” aliendelea kusimulia.

Pia aliamua kuficha siri hiyo kwa mamaye. Alifahamu angehusika kumshawishi aweze kurejea kwenye ndoa hiyo. Mwanawe ambaye sasa ana umri wa miaka 4, ameamua atazidi kuwa msiri.

“Najutia mbona nafanya… Wakati utafika wa kufanya maamuzi yakuridhisha,” alisema Wanja.

Mwanasaikolojia Jane Ngatia, anasema matukio haya yanafanyika na wanaume wengi wamenyimwa nafasi ya kulea wanao.

Bi Ngatia amesema wanaume ambao wanafanya majukumu kama yale, wamenyimwa haki ya kufikiria.

“Hayo sio maadili mema ya kuchukua pesa za wanaume wengine kulisha watoto ambao wana baba yao. Huo ni wizi ambao unaendelezwa na wanawake,”alisema mwanasaikolojia huyo.

  • Tags

You can share this post!

Polisi wa cheo cha juu aumizwa na mdogo wake katika zogo la...

Ziara ya Mfalme: Ruto na Rigathi lawamani kwa kunyamazia...

T L