• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 6:55 AM
Polisi wa cheo cha juu aumizwa na mdogo wake katika zogo la ‘printer’ ya ofisi

Polisi wa cheo cha juu aumizwa na mdogo wake katika zogo la ‘printer’ ya ofisi

Na CECIL ODONGO

Katika tukio la kushangaza, afisa wa polisi katika Kaunti ya Kericho mwishoni mwa mwezi uliopita  alimpiga bosi wake baada ya mzozo kuibuka kuhusu matumizi ya tarakilishi na kichapishi (printer) kituoni mwao.

Ripoti ya polisi inasema afisa huyo wa cheo cha konstebo Gideon Kipng’etich anayehudumu katika kituo cha polisi cha Booker, alimvurumishia bosi wake wa cheo cha ‘Senior Sergent’ Caleb Manani makonde mazitomazito wakati wa ugomvi kati yao.

Siku ya tukio ambayo ni Oktoba 31, Bw King’etich alimpigia Bw Manani simu akimuuliza kwa nini alisema kuwa ndiye alitumia tarakilishi na kichapishi cha afisi ambacho baadaye ilibainika kimeharibika.

Bw Manani alikuja afisini na kumkabili mdogo wake ndipo wakagombana vikali.

Hapo ndipo Bw Kipng’etich alimsukuma bosi wake chini kisha akamvamia kwa mangumi mazito mazito, hali ambayo ilimwacha na majeraha mabaya usoni. Alikimbizwa hadi Hospitali ya Kericho ambako alitibiwa kisha na kuruhusiwa kuenda nyumbani.

Wakati walipokuwa wakipigana, wawili hao waliharibu kichapishi aina ya L3110 ambacho thamani yake ni Sh30,000. Taarifa hiyo ilieleza kuwa kisa hicho kilikuwa kikiendelea kuchunguzwa.

Soma pia: https://taifaleo.nation.co.ke/habari-mseto/vizuizi-vya-polisi-vingali-barabarani-licha-ya-marufuku-ya-waziri-kindiki

  • Tags

You can share this post!

Demu jirani yangu huteswa na mumewe, nashawishika kumnusuru...

Jinsi wanaume wanavyolaghaiwa na wanawake ili kulea watoto...

T L