• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Kaizer Chiefs anayochezea Mkenya Akumu mguu mmoja fainali ya Klabu Bingwa

Kaizer Chiefs anayochezea Mkenya Akumu mguu mmoja fainali ya Klabu Bingwa

Na GEOFFREY ANENE

KAIZER Chiefs iliduwaza Wydad Casablanca 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu-fainali na kuweka hai matumaini ya kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika na tuzo ya bingwa ya Sh269.5 milioni, Jumamosi.

Chiefs, ambayo iliingiza kiungo Mkenya Anthony Akumu katika nafasi ya mshambuliaji wa Colombia Leonardo Castro dakika ya 80, ilipata ushindi huo muhimu kupitia bao la Samir Nurkovic. Mshambuliaji wa Serbia, Nurkovic alitikisa nyavu za Wydad dakika ya 34 baada ya kupokea mpira kutoka kwa beki Njabulo Blom.

Kocha Arthur Zwane ameeleza tovuti ya klabu ya Chiefs kuwa kazi kubwa bado ipo ya kufanywa katika mechi ya marudiano mnamo Juni 25 nchini Afrika Kusini.“Tulikuja hapa kufanya kazi na tulifanya vivyo hivyo. Tunafurahia matokeo, lakini tunajua kuwa mambo bado.

Tutakuwa wenyeji wa mechi ya mkondo wa pili mjini Johannesburg na tutajaribu kukamilisha kazi huko,” alisema Zwane baada ya ushindi huo wa kihistoria.Chiefs pia itashukuru kipa Bruce Bvuma kurejea nyumbani na ushindi. Alifanya kazi kubwa michumani. Wydad ilivamia ngome ya Chiefs kama nyuki.

“Kila mtu alijitolea asilimia 100. Nimefurahia matokeo na pia kutofungwa bao. Tunajua kuwa kibarua kimefika tu mapumzikoni. Lazima tuendelee kufanya bidii,” alishauri Bvuma.Chiefs ikafaulu kubandua Wydad, itakutana na mshindi kati ya miamba wa Tunisia Esperance na mabingwa watetezi Al Ahly kutoka Misri.

Al Ahly ililaza Esperance 1-0 mjini Tunis mnamo Juni 19. Itaalika klabu hiyo ya Tunisia mjini Cairo mnamo Juni 25. Nambari mbili itazawadiwa Sh134.7 milioni. Timu zitakazopoteza katika nusu-fainali zitapokea Sh94.3 milioni kila moja.

  • Tags

You can share this post!

Okumbi kuongoza Harambee Stars U23 Cecafa

Shujaa na Lionesses kufahamu makundi yao ya Olimpiki