• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 1:02 PM
‘Kaunti jirani zipige jeki Coast General’

‘Kaunti jirani zipige jeki Coast General’

NA JURGEN NAMBEKA

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imeeleza hitaji la serikali za kaunti jirani kuchangia rasilimali kwa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Pwani iliyoko kaunti hiyo.

Gavana wa Mombasa, Bw Abdulswamad Nassir, alisema hatua hiyo imependekezwa na kamati za bunge la kaunti za afya na leba, ili kuboresha utoaji huduma kwa wakazi wanaotegemea hospitali hiyo.

“Ilitambuliwa kuwa, Hospitali Kuu ya Rufaa ya Pwani huhudumia Pwani nzima kwa hivyo itakuwa vyema iwapo kaunti zingechangia rasilimali ili kushughulikia mapungufu yanayokumba hospitali hiyo,” akasema Bw Nassir.

Ripoti za kamati hizo zilieleza kuna changamoto kubwa ya uhaba wa wahudumu wa afya katika hospitali hiyo.

Bw Nassir aliongoza mkutano wa kamati hizo kutafuta namna ya kuvutia wahudumu ili kuboresha utoaji huduma za afya.

Katika miaka iliyopita, kaunti hiyo ilikumbwa na changamoto za ulipaji mishahara kwa wahudumu wa afya, ambapo kulikuwa na migomo ya mara kwa mara.

Hata hivyo, Bw Nassir alipoingia mamlakani aliweka mkataba na shirika la fedha liwe likiwalipa wafanyakazi mishahara kwa mkopo ambao kaunti hulipia badaye.

  • Tags

You can share this post!

Ushindi wa Wanjiru waipa Kenya dhahabu ya 3 Poland

TAHARIRI: Ni fedheha wanasiasa kufadhili wahuni

T L