• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Kaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo

Kaunti yafadhili 300 kuhudhuria mazishi ya mzee wa jamii ya Waluo

NA MKAMBURI MWAWASI

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa imewafadhili watu 300 kutoka jamii ya Waluo kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la jamii hiyo Mzee Willis Otondi (Ker), yatakayofanyika Nyahera, Kaunti ya Kisumu leo Jumamosi.

Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir, pia anatarajiwa kujiunga na waombolezaji hii leo Jumamosi, kwa mazishi hayo.

Mwenyekiti wa jamii ya Waluo eneo la Nyali, Bw Kings Obara, alisema kwamba mzee Otondi, alikuwa tegemeo kubwa kwa jamii hiyo.

Kulingana naye, alikuwa mpatanishi endapo kungeibuka vita nchini na alitoa huduma za kutafsiri mila na tamaduni za wajaluo.

“Tulimuomba gavana atusaidie ili tuweze kufika na kumpumzisha mzee wetu. Ker ni kama kuchagua pope wa kanisa la kikatoliki. Wazee huenda sehemu ya Gotramogi wanapiga kambi kama siku tatu kumteua,” alisema Obara.

Mzee Otondi alifariki Februari 17 baada ya kuugua kwa muda mrefu katika hospitali ya rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga jijini Kisumu.

  • Tags

You can share this post!

Pigo kwa ODM wabunge wawili wakipoteza viti vyao

DOUGLAS MUTUA: Kweli Kenya imehalalisha ushoga au ni hisia...

T L