• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
Kiambu yaendelea kujiimarisha katika ufugaji wa samaki

Kiambu yaendelea kujiimarisha katika ufugaji wa samaki

Na LAWRENCE ONGARO

IDARA ya uvuvi kwa ushirikiano na Kaunti ya Kiambu imezindua ufugaji wa samaki katika bwawa la Rugiri, kaunti ndogo ya Kabete.

Tayari idara hiyo inalenga kuzuru maeneo tofauti kuzindua mabwawa manane ambapo samaki wapatao 80,000 watafugwa.

Waziri wa kilimo kaunti hiyo Bw Joseph Kamau, alisema wamezindua mradi huo kwa sababu mara nyingi wakazi wa Kiambu wametaka mwongozo ili waweze kufuga samaki kwa wingi.

“Wakazi wengi wa eneo hilo wameanza kukumbatia ufugaji wa samaki huku wengi wakitarajia kujiendeleza na mradi huo.

Alisema kaunti ya Kiambu itaendelea kushindana na maeneo ya Nyanza ambako samaki hupatikana kwa wingi.

“Tunawaomba wakazi wa Kiambu wazingatie ufugaji wa samaki katika maeneo mengine ili watu wengi wajitoee kuona ya kwamba samaki wanavuliwa kwa wingi,” akasema.

 

Aliahidi atazuru maeneo mengine ili kuwashauri wananchi wafuge samaki kwa wingi.

Alisema uchumi wa Kiambu utaimarika haraka huku pia ulaji wa samaki ukiongezeka maradufu.

Alisema serikali iko tayari kuwatafutia soko sehemu tofauti baada ya kuvua samaki hao.

” Kila mfugaji wa samaki atalazimika kufanya bidii ili kufanikisha mradi huo ambao unakuja kwa kasi katika eneo la Kati,” alisema waziri huyo.

  • Tags

You can share this post!

Matumaini kiungo Jack Grealish wa Aston Villa atacheza...

Kilio beste akiponyoka na bebi wake