• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Kijakazi akiri kuiba Sh1 milioni za mwajiri wake mgonjwa

Kijakazi akiri kuiba Sh1 milioni za mwajiri wake mgonjwa

NA JOSEPH NDUNDA

Kijakazi amekiri kwamba aliiba Sh1 milioni za mwajiri wake aliyekuwa akiugua jijini Nairobi.

Bi Roseline Kahega alikamatwa na polisi katika Kaunti ya Kericho akielekea nyumbani kwao mashambani Kaunti ya Vihiga baada ya kuiba pesa hizo kutoka kwa mwajiri wake Libin Abdi Mohamed mtaani Eastleigh mnamo Oktoba 13.

Bi Mohammed alikuwa amekusanya pesa hizo kugharamia upasuaji ng’ambo.

Mlalamishi ambaye anaugua anatarajiwa kusafiri kwenda India kwa upasuaji na alikuwa amechanga pesa hizo kutoka kwa jamaa na marafiki na kuziweka katika nyumba yake akisubiri tarehe ya kusafiri.

Alianza kumwajiri Bi Kahenga kwa muda kusafisha nyumba. Siku ya tukio, Bi Kahenga hakufika kazini na alipompigia simu ilikuwa imezimwa na akaamua kuthibitisha iwapo kila kitu kilikuwa sawa ndani ya nyumba. Ni wakati huo ambapo aligundua pesa zake zilikuwa zimeibwa.

Bi Mohammed alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha California na maafisa wa usalama wakaanza uchunguzi kwa kuthibitisha waliokuwa wamepanga kusafiri wakitumia magari ya uchukuzi wa umma kuelekea Vihiga kutoka Nairobi na kugundua kwamba Bi Kahega alikuwa amependa basi kuelekea kwao mashambani.

Alikamatwa akiwa Kericho na kurudishwa Nairobi kushtakiwa. Alikiri mashtaka mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Makadara Mary Njagi na akazuiliwa rumande hadi Oktoba 25 atakapohukumiwa baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha eksibiti kortini.

  • Tags

You can share this post!

Amerika yaambia kampuni, raia wake wasianzishe biashara...

Esther Musila afurahia tuzo ya kufanya kazi UN kwa muda...

T L