• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Amerika yaambia kampuni, raia wake wasianzishe biashara Uganda

Amerika yaambia kampuni, raia wake wasianzishe biashara Uganda

NA MASHIRIKA

WASHINGTON, AMERIKA

WIZARA za Masuala ya Nje, Ajira, Afya na Huduma za kibinadamu, Biashara, na shirika la Maendeleo la Kimataifa la Amerika (USAID), Jumatatu zilitoa tahadhari ya kufanya biashara na Kampala.

Tahadhari hiyo inazifahamisha kampuni za kibiashara na watu binafsi wa Amerika, wakiwemo mashirika ya huduma za afya, maafisa wa taasisi za kitaaluma na wawekezaji, kuhusu athari zinazoweza kuwakabili ikiwa watafanya biashara nchini Uganda.

“Biashara, mashirika na watu binafsi wanapaswa kufahamu athari zinazoweza kutokea za kifedha na sifa, zinazotokana na ufisadi uliokithiri, uliofafanuliwa kwa undani zaidi katika taarifa ya hali ya uwekezaji ya 2023,” ripoti hiyo ilisoma.

Mambo yaliyoelezwa kwenye ripoti hiyo yanayjumuisha unyanyasaji dhidi ya wanaharakati wa haki za binadamu, wanahabari, wafanyakazi wa afya, watu wa makundi ya walio wachache, watu wa kundi la LGBTQI+, na wapinzani wa kisiasa.

Haya yanajiri miezi minne tu baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutia saini sheria ya kuharamisha ushoga nchini humo.
Kufuatia hatua hiyo, Uganda ilikashifiwa na kupokea shinikizo la kubadilisha msimamo huo.

Hata hivyo, Museveni alishikilia kuwa sheria hiyo inalenga kulinda utamaduni wa wakazi wa Uganda.

Mnano Mei, Rais wa Amerika, Joe Biden, alisema kuwa kuharamisha ushoga ni ishara tosha kuwa Uganda inakiuka haki za binadamu.

Kadhalika, Biden alionya kuwa hatua hiyo ingehatarisha maendeleo ya uchumi wa Uganda.

“Ninaungana na watu duniani kote wakiwemo watu wengi wa Uganda katika kuitaka sheria hiyo ifutwe mara moja.

“Hakuna mtu anayestahili kuishi kwa kuhofia maisha yake wakati wote au kufanyiwa vitendo vya ukatili na ubaguzi. Ni makossa,” Biden alisema wakati huo.

Kadhalika, Benki ya Dunia ilisitisha ufadhili wake nchini Uganda, kutokana na sheria hiyo tata.

  • Tags

You can share this post!

Mtoto aaga dunia kwa kukosa kuhudumiwa hospitalini kwa saa...

Kijakazi akiri kuiba Sh1 milioni za mwajiri wake mgonjwa

T L