• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 2:12 PM
Kijana ajeruhiwa baada ya kushambuliwa na kiboko

Kijana ajeruhiwa baada ya kushambuliwa na kiboko

Na ALEX KALAMA

KIJANA mwenye umri wa miaka 19 amelazwa katika Hospitali Kuu ya Malindi, Kaunti ya Kilifi baada ya kujeruhiwa vibaya na kiboko karibu eneo la jumba la utafiti la Chuo Kikuu cha Moi katika Wadi ya Sabaki.

Imesemekana Elias Emmanuel Bemahango alikuwa na wenzake wawili wakitimbea na walipofika eneo hilo, ghafla kiboko aliyekuwa na mwingine mdogo akawashambulia. Wenzake wawili walifanikiwa kutoroka.Bw Stembo Kaviha ambaye ni mjomba wake, mwathiriwa alipata majeraha mabaya tumboni na mgongoni.

Bw Kaviha aidha ameitaka serikali kuruhusu mtu anayeshambuliwa na wanayama pori aweze kutibiwa kwanza kisha baadaye taratibu za kuandikisha taarifa zifuate, akidai kijana huyo alichelewa kupokea matibabu akiambiwa kwanza aonyeshe taarifa za shirika la huduma za wanyamapori nchini (KWS).

Naibu Chifu wa kata ndogo ya Sabaki, Bi Rachael Malingi alithibitisha kisa hicho akisema aliwasiliana na maafisa wa KWS ili kutathimini kisa hicho ili kubaini ni fidia gani atakayowezwa kulipwa mwathiriwa.

Bi Malingi aidha ametoa wito kwa wakazi wa maeneo ambayo yanapakana na mto Sabaki kuwa waangalifu kutokana na viboko kuingia vijijini wakitafuta chakula baada ya viboko hao kumaliza mimea.Hata hivyo amewataka wakazi kupiga simu mara moja kwa maafisa wa huduma kwa wanyama pori nchini wanapowaona wanyama wakizurura vijijini.

  • Tags

You can share this post!

Maafisa wawasaka majambazi walioua mfanyabiashara mtaani

Bitok kuchuja kikosi cha Malkia Strikers