• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Kikosi spesheli kutumwa Tana River na Lamu

Kikosi spesheli kutumwa Tana River na Lamu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki akiwa katika eneo la Wayu, Galledyertu katika Kaunti ya Tana River,ametangaza kwamba serikali itatuma kikosi spesheli cha katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi na ukanda wa juu wa pwani kukabiliana na magaidi.

“Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba maafisa wetu wanapata silaha vifaa vya kiteknolojia vitakavyowapa uwezo wa kukabiliana na wahalifu,” amesema waziri Kindiki akiahidi kwamba wanaotumia silaha ipasavyo ili kujilinda nao wataendelea kuungwa mkono kikamilifu.

Amezitaka jamii jirani kuendelea kuishi bila kuzozana na endapo kutatokea mgogoro waachie serikali na taasisi huru kama idara ya mahakama fursa ya kutatua kesi.

Amewataka maafisa wa utawala kuhakikisha wanatekeleza kazi yao kwa uadilifu bila kuegemea upande wowote.

Amesema kuanzia Oktoba 1, 2023, serikali itatuma mwanakandarasi kujenga makao ya utawala katika eneo la Galledyertu.

Gavana wa Tana River Godhana Dhadho, Seneta Danson Mungatana, wabunge, madiwani na mshirikishi wa pwani pamoja na kamati za kiusalama wamehudhuria kikao cha baraza kuangazia suala la usalama.

Kauli ya waziri inajiri saa chache baada ya shambulio kutokea katika eneo la Widho-Mashambani, Lamu Magharibi ambapo bawabu ameuawa na Al-Shabaab walioteketeza nyumba tano.

  • Tags

You can share this post!

DCI kutoka makao makuu wafika Mombasa kuchunguza kifo cha...

Wito mashamba makubwa ya kilimo yalindwe kazi zisipotee

T L