• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:55 PM
Kinoti akwepa hukumu

Kinoti akwepa hukumu

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa Uchunguzi wa Jinai (DCI) George Kinoti Jumatatu alikwepa kufika kortini kuhukumiwa kwa kukaidi agizo la  mahakama kuu.

Bw Kinoti alikaidi agizo la Feburuari 14 2021 arudishe bastola na bunduki saba kwa mfanyabiashara Jimmy Wanjigi anayemezea mate kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha ODM.

Bw Kinoti alikuwa amepewa hadi Machi 25, 2021 amrudishie Wanjigi silaha zilizotwaliwa na maafisa wa polisi kutoka kwa makazi yake Nairobi na Malindi 2017.Jaji Antony Mrima alimwagiza DCI arudishe silaha hizo kwa vile Bw Wanjigi alikuwa na leseni za kuzimiliki silaha hizo.

Jaji Mrima alimpa Kinoti siku 30 kutekeleza agizo hilo la mahakama.Jaji Enock Mwita alimpata na hatia Bw Kinoti ya kukaidi agizo la mahakama .Kinoti alikuwa ameomba muda hadi Septemba 27,2021.Kinoti hakufika kortini na hakurudisha silaha hizo.

Wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo Jumatatu ,korti iliamuru iendelee faraghani kwa madai kulikuwa na habari mahususi ambazo umma haupasi kuelezwa.Kinoti alipokosa kufika kortini Jumatatu , Jaji Antony Mrima, aliahirisha kesi hadi Novemba 18, 2021 atakapopitisha adhabu.

Mahakama haikuelezwa sababu ya Bw Kinoti kufika kortini.Akiwahutubia wanahabari Bw Wanjigi alisema familia yake iliteseka sana wakati wa maafisa wa DCI walipovamia familia yake.

  • Tags

You can share this post!

Masharti kwa makocha wa soka Kenya

Arsenal wazamisha chombo cha Spurs ligini