• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 11:30 AM
Maafisa watatu wakuu wa polisi kujua hatma yao octoba 28

Maafisa watatu wakuu wa polisi kujua hatma yao octoba 28

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya Milimani Nairobi itaamua Oktoba 28 iwapo itawasukuma maafisa watatu wakuu wa polisi kwa kukaidi agizo la kumwachilia Mbunge wa Gatundu kusini Moses Kuria aliyekuwa amezuiliwa kwa kumpiga na kumwumiza mwanamke.

Agizo la kuachiliwa kwa Bw Kuria  ilikuwa imetolewa Januari 10 2020 na hakimu mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot. Bw Cheruiyot alikuwa amewaagiza OCPD wa Kilimani Bw Aden Mohammed na afisa anayesimamia idara ya uchunguzi wa jinai DCIO Fatuma Hadi na OCS wa Kilimani.

Akiomba maafisa hao watatu wa polisi wafungwe jela wakili Geoffrey Omenge alisema maagizo ya mahakama yapasa kuheshimiwa na kutekelezwa.

“Naomba hii mahakama iwasukume jela Bw Mohammed , Bw Hadi na naibu wa mkuu wa kituo cha polisi cha Kilimani kwa kukaidi agizo la mahakama la Januanuari 10,2020,”  Bw Omenge alisema.

Wakili huyo alieleza mahakama maafisa wa polisi wanaopasa kuwa msitari wa mbele kutii na kutekeleza maagizo ya mahakama.“Badala ya watatu hao OCPD , DCIO na naibu wa OCS kutekeleza maagizo ya mahakama na kumwachilia Bw Kuria walipuuza agizo hilo,”alisema Bw Omenge.

Wakili huyo alisema OCPD alitusi mahakama aliposema “agizo lake ni karatasi tu na hana budi kuikaidi.” Alisema ikiwa afisa mkuu wa polisi anaongoza katika tabia ya kukaidi agizo la mahakama basi wananchi wa kawaida hawataziheshimu kamwe kwa vile hakuna yeyote wa kuitekeleza.

Mahakama pia ilielezwa nchi hii itakuwa haitawaliwiki kwa utovu wa nidhamu endapo maafisa wa polisi wanaopasa kutekeleza maagizo ya mahakama ndio watakaokaidi maagizo ya mahakama.

Bw Omenge alisema ushahidi aliowasilisha umethibitisha kabisa kwamba OCPD , DCIO na OCS ndio walikaidi agizo la mahakama. Alisema badala ya kumwachilia Bw Kuria walimzuilia korokoroni na watu wa familia yake na wakili wake pamoja na wanasiasa walirushiwa hewa ya kutoa machozi walipoenda kumwona mwanasiasa huyo korokoroni pamoja na kuwakabidhi OCPD ,DCIO na naibu wa OCS nakala ya agizo  la mahakama.

Bw  Cheruiyoti alielezwa “OCPD aliamuru maafisa hao wakuu wa polisi wawatwange wanasiasa na mawakili nchi.” Hatimaye OCPD alimwachilia Bw Kuria kwa dhamana ya Sh20,000 ilhali alikuwa ameachiliwa na hakimu  kwa dhamana ya Sh50,000.

Lakini wakili wa serikali Bw Martin Munene aliomba mahakama itupilie mbali kesi hiyo akisema haiambatani na vipengee vya sheria na liliwasilishwa kuwaahibisha maafisa hao wa polisi.

  • Tags

You can share this post!

Ruto, Muturi wasuta mabwanyenye wa MKF kwa kudai ndio wenye...

Mwenye mazoea ya kuibia wenye maduka ya Mpesa achapwa kama...