• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Maduka yaanza kukataa ‘Lipa Na Mpesa’ sababu ya ushuru wa juu

Maduka yaanza kukataa ‘Lipa Na Mpesa’ sababu ya ushuru wa juu

NA LABAAN SHABAAN

SEHEMU ya maduka yameanza kukataa huduma ya malipo kwa njia ya simu ‘Lipa na Mpesa’ wakihepa ada ya juu ya kuwezesha ununuzi.

Taifa Leo Digital imeona mabango madukani yanayowazuia wateja kulipia huduma kwa njia ya simu yakitaja ongezeko la gharama ya muamala kati ya simu na benki.

Moja ya maduka yaliyopiga breki ‘Lipa na Mpesa’ limejumuisha kitengo cha biashara ya kutoa na kutuma pesa kwa njia ya Mpesa katika shughuli zake za biashara.

Wateja hapa wanahitajiwa kutoa pesa kama njia ya kulipia huduma na bidhaa. Vinginevyo, wawezeshe biashara kwa mfumo wa pesa taslimu.

Kwa njia hii mwanabiashara huyu atapata faida maradufu.

Moja ni kupitia huduma ya pesa, na ya pili ni kuuza bidhaa ama huduma aliyoweka dukani mwake.

Ilani katika duka hili inasema, “Kwa sababu ya kupanda kwa gharama ya muamala kupitia simu na benki, hatutaruhusu malipo kupitia ‘paybill’ na ‘buy goods’ kutoka Oktoba 1, 2023. Tafadhali lipa kwa pesa taslimu ama utoe pesa.”

Gharama ya ada ya huduma ya pesa kupitia simu imepanda kwa sababu ya kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha ya 2023.

Sheria hiyo ilipandisha ushuru wa bidhaa kutoka asilimia 12 hadi 15.

Tukio hili lilisukuma kampuni za mawasiliano kuratibu upya ada za kuhamisha pesa kwa njia ya simu.

  • Tags

You can share this post!

Kinyanjui ajinyanyua mwaka mmoja baada ya kulambishwa...

Kasisi wa Afrika Kusini anayeacha mabinti wa Kenya na kiu...

T L