• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Maisha ya binadamu yana thamani kuliko maua, Sifuna amwambia Murkomen

Maisha ya binadamu yana thamani kuliko maua, Sifuna amwambia Murkomen

NA WINNIE ONYANDO

SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna amelaani hatua ya Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen ‘kuomboleza’ maua yaliyoharibiwa katika barabara ya Nairobi Expressway mnamo Jumatano wakati wa maandamano.

“Tuliona waziri Kipchumba Murkomen akiomboleza maua yaliyoharibiwa katika Expressway siku ya maandamano. Je, atalinganisha vipi thamani ya binadamu na maua?” Sifuna akauliza.

Seneta huyo amesema kuwa waziri Murkomen anafaa kuangazia suala la watu kupoteza maisha badala ya kushughulikia maua ya Expressway.

Hata hivyo, amesema kuwa kama muungano, wanalaani uharibifu uliotokea wakati wa maandamano ya Jumatano wiki hii.

Mnamo Ijumaa, viongozi wa Azimio wamewatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kihumbuini ambao walirushiwa gesi za kuwatoa machozi wakati wa maandamano Jumatano wiki hii.

Bw Sifuna ametembelea shule ya Kihumbuni akiandamana na Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi na mwenzake wa Embakasi Mashariki Babu Owino.

Haya yanajiru siku moja tu baada ya waziri Murkomen kukadiria hasara ya uharibifu uliofanywa katika barabara ya Nairobi Expressway kuwa ni wa Sh700 milioni.

  • Tags

You can share this post!

Kanini Kega adai Raila na Kenyatta ndio walisababisha...

Tatuwasco yapokea tuzo kwa usambazaji mzuri wa maji

T L