• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:01 PM
Mamake Tecra jinsi mamilioni yake yalipelekewa Omar Lali

Mamake Tecra jinsi mamilioni yake yalipelekewa Omar Lali

Na RICHARD MUNGUTI

UCHUNGUZI wa kubaini kilichosababisha kifo cha Patricia Tecra Wangari, bintiye wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza pombe cha Keroche Brewery Limited ulianza kusikizwa Jumanne huku mahakama ikielezwa mpenziwe marehemu alikuwa amepokea zaidi ya Sh500,000 kutoka kwa Tecra.

Bi Tabitha Muigai, mama yake Tecra, alieleza mahakama kuwa Bw Omar Lali, mpenziwe marehemu alikuwa anatumiwa pesa katikia mtandao wa Mpesa na pia kutoka kwa Benki ya Absa.

Kati ya Septemba 2019 na Machi 2020 Bw Lali alikuwa amepokea zaidi ya Sh500,000 kutoka kwa Tecra.

Ushahidi huo wa mama yake Tabitha uliungwa mkono ni aliyekuwa msaidizi wa Tecra, Bi Sarita Ikenye alimweleza hakimu mwandamizi Bi Zainab Abdul kwamba ndiye alikuwa anamtumia Bw Lali pesa.

“Je ulijua pesa hizo ulizokuwa unatuma kwa Bw Lali zilikuwa za kufanyakazi gani,” kiongozi wa mashtaka Bw Peter Muia alimwuliza Bi Ikenye.

“Hapana sijui zilikuwa za nini. Pia nilikuwa namtumia Bw Eric Cheruiyot, dereva wa Tecra,” alijibu Bi Ikenye.

Msaidizi huyo wa Tecra aliwasilisha mahakamani nakala za ushahidi kutoka benki ya ABSA na kampuni ya Safaricom.

Tecra aliaga mnamo Mei 2020 katika Nairobi Hospital alipokuwa anapokea matibabu. Alisafirishwa kwa ndege ya Amref kutoka Lamu baada ya kuumia.

Tabitha alisema ni Bw Lali aliyepiga simu kueleza Tecra ameanguka na kupata majeraha ya kichwa mnamo Aprili 22 2020.

Mama huyo alisema Tecra ndiye alimfichulia alikuwa ameachumbiana na Bw Lali mwenye umri wa miaka 50. “Tecra alinionyesha picha za Bw Lali na mara moja nikamweleza alikuwa mkubwa kumliko kiumri,” Tabitha alieleza korti.

Katika taarifa aliyotoa kwa polisi baada ya Tecra kufariki , Tabitha alifichua kwamba familia ilikuwa imeukataa urafiki wake na Bw Omari Lali.

“Familia ilimtaka Tecra avunje urafiki wakehuo na Bw Lali,” alisema Tabitha.

Tecra,30, alikataa kuuvunja na kuwakataza watu kuenda katika makazi yake mjini Naivasha kwa vile alikuwa akiishi na Bw Lali. Bw Lali alikuwa 50 na Tecra alikuwa na umri wa miaka 30.

Bi Muigai aliyeandamana na mumewe Bw Joseph Muigai Karanja, alisema , Tecra alienda kuishi Lamu kwenye hoteli akiwa na Bw Lali.

“Tulizugumza na Tecra kwenye hoteli mjini Naivasha na kisiwani Lamu.Nilimwona Bw Lali kwa mara ya kwanza Lamu. Alikuwa na umri mkubwa,” alisema Tabitha.

Mahakama ilielezwa baada ya Bw Lali kudokeza Tecra ameumia na yuko hospitali , mipango ilifanywa na kumsafirisha hadi Nairobi. Bw Lali aliandamana na madaktari wa Amref waliomsafirisha Tecra kutoka Lamu.

Alimkabidhi , Tabitha simu ya Tecra. Uchunguzi utaendelea leo.

  • Tags

You can share this post!

Visa vya wanahabari kuendelea kuhangaishwa na maafisa wa...

Mpenziwe Tecra alimtishia mlinzi, mahakama yaambiwa