• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:55 AM
Mjane akimbilia mahakama kunusuru kipande cha ardhi

Mjane akimbilia mahakama kunusuru kipande cha ardhi

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imesitisha ujenzi wa  taasisi ya elimu inayodhaminiwa na Ubalozi wa Uturuki katika ardhi ya ukubwa wa ekari 10 inayodaiwa inayodaiwa kunyakuliwa kutoka kwa mjane.

Jaji Millicent Akinyi Odeny alisimamisha ujenzi wa taasisi ya Holistic Educational Trust hadi kesi iliyoshtakiwa na Bi Daula Mohammed Omar isikilizwe na kuamuliwa.

Jaji Odeny alisema ushahidi uliowasilishwa na wakili Michael Oloo anayemtetea Daula umedhihirisha shamba hilo lilinyakuliwa 2016 kisha mnyakuzi akauzia taasisi hiyo ya Holistic.

Ujenzi wa taasisi hiyo ya elimu ya juu ukikamilika, wanafunzi zaidi ya 1,000 watasajiliwa kusomea shahada mbali mbali.

Bw Oloo alimsihi Jaji Odeny asitishe ujenzi wa taasisi hiyo hadi kesi aliyowasilisha Daula isikilizwe.

Jaji Odeny alielezwa kwamba mjane aliuziwa shamba hilo la ekari 10 na Abdalla Hemed mnamo 2014 kwa bei ya Sh1.5 milioni lakini ajenti wake Khalid Mohamed Ali akalisajili kama lake.

Khalid aliuzia Khalfan Mohammed Abdalla Rafrouf shamba hilo naye akaliuza kwa Holistic.

Kesi hiyo itasikilizwa Septemba 26, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni iliyomulikwa kuanika wanawake uchi yaomba msamaha

SIKU YA KISWAHILI DUNIANI: Sherehe kufana miji ya ndani na...

T L