• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Museveni adai wanaokula kuku huwa na mienendo hafifu

Museveni adai wanaokula kuku huwa na mienendo hafifu

NA WINNIE ONYANDO

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni ameeleza kwamba aliacha kula nyama ya kuku, samaki, nguruwe na nyama ya kondoo kwa sababu watu wanaokula vyakula kama hivyo wana mienendo hafifu.

Japo rais huyo alikosa kutoa maelezo kamili kuhusu suala la kutokula vyakula kama hivyo, aliwataka raia wake kuheshimu imani ya kila mtu.

“Nguruwe ni haramu, samaki ni haramu kwangu… Sili kuku kwa sababu unapokula nyama ya kuku unakuwa na mienendo hafifu. Kuku ni ndege. Sili nyama ya kondoo, sili vitu hivyo vyote na kwa hivyo orodha ya vyakula ambavyo sili ni ndefu zaidi,” akasema Rais Museveni.

“Tofauti na sisi hapa, na watu wa eneo hili, ni kwamba imani yoyote niliyo nayo, simwekei vikwazo jirani yangu ikiwa ana imani tofauti,” akaongeza Bw Museveni.

Kadhalika, rais huyo alitoa mfano wa jamii zinazojiepusha na ulaji wa nyama ya kuku wakati wakiendelea kufuga ndege hao.

Museveni aliwashauri raia wa Uganda kutokiuka imani ya mtu mwingine au kujaribu kuwawekea wenzao vikwazo.

“Kwa mfano, ingawa Banyankole walikuwa hawali kuku, walikuwa wakifuga kuku kwa ajili ya sherehe za kitamaduni. Hata hivyo, kila mmoja ana imani yake. Lazima tuheshimu imani ya mwingine.”

  • Tags

You can share this post!

Shule yapata darubini, vifaa vingine sayansi ikigeuzwa...

Siri ya familia ya Kenyatta yafichuliwa

T L