• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:07 PM
Mwago sasa adai baadhi ya machifu Starehe ni ‘maadui’ wa maendeleo

Mwago sasa adai baadhi ya machifu Starehe ni ‘maadui’ wa maendeleo

NA SAMMY KIMATU

MAAFISA wa utawala na wazazi wameombwa kuangazia elimu ya mtoto kuliko kuyapa kipaumbele masuala ya siasa.

Akiongea na Taifa Leo mnamo Jumanne, Mbunge wa Starehe Amos Mwago Maina aliambia naibu kamishna wa Starehe Bw John Kisang kwamba awasihi machifu wampatie nafasi ya kuwafanyia wakazi wa Starehe kazi badala ya kujishughulisha na siasa.

“Bw Kisang, tafadhali waambie machifu waachane na siasa. Kampeni na kura zilimalizika na wakati huu naomba kupewa nafasi ya kuwafanyia wakazi wa Starehe kazi,” Bw Mwago akasema.

Licha ya hayo, Bw Mwago aliwahakikishia wazazi kwamba atafanya kila juhudi kama kiongozi wao kuona kwamba amepiga jeki watoto kuhakikisha wamepata elimu.

Aliongeza kwamba kuna hazina ya kitaifa ya kufadhili elimu kupitia usambasaji wa basari.

“Ni haki ya kila mtoto kupata elimu. Pale kidogo mzazi atalemewa kwa upande wa karo, tutatumia nafasi na uwezo wetu kutoa basari ili mtoto asome,” Bw Mwago akatoa hakikisho.

Vile vile, mbunge huyo wa muhula wa kwanza, alishauri wazazi kumakinika na kuhakikisha usalama wa watoto wao hasa wakati huu ambapo watoto wako kwa likizo ndefu.

Kadhalika, alisema ni makosa watoto kuonekana wakirandaranda sokoni au mtaani.

  • Tags

You can share this post!

Wanasiasa wa UDA North Rift waelezea matumaini ya uchaguzi...

‘Tiktoker’ Azziad Nasenya apuuzilia mbali uvumi...

T L