• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 9:59 AM
Mwanamke alilia korti imsaidie kupata Sh29m kutoka kwa sacco

Mwanamke alilia korti imsaidie kupata Sh29m kutoka kwa sacco

NA BRIAN OCHARO

MWANAMKE mmoja mjini Mombasa, ameililia mahakama imsaidie kuokoa Sh29 milioni anazodai aliweka katika chama cha ushirika kwa matumaini ya kupata riba tele, lakini zikapotea.

Bi Claudia Mueni, ameambia Mahakama ya Rufaa ya Mombasa kuwa, alihamisha pesa hizo kutoka Benki ya Kenya Women Finance Trust (KWFT) hadi FEP Sacco Society Ltd katika mwaka wa 2019.

Juhudi za kutaka kulipwa pesa hizo ziligonga mwamba, alipopeleka kesi katika Mahakama Kuu awali.

Kulingana na hati alizowasilisha mahakamani, alisema alilipwa Sh1.1 milioni pekee kinyume na matarajio yake.

Kwa upande wake, Sacco ya FEP imeshikilia kuwa, mwanamke huyo alikuwa mwanachama wake baada ya kuwasilisha ombi lake mwaka wa 2019.

Afisa Mkuu wa Sacco hiyo, Dkt Jackson Wanjau, alisisitiza kuwa mwanamke huyo alikuwa mwanachama baada ya kutuma maombi na kujaza fomu kabla ya fedha hizo kuhamishwa.

Hata hivyo, aliiambia mahakama kuwa baadaye mlalamishi alijiondoa kwenye sacco hiyo kwa kujaza fomu za lazima za kujitoa.

Katika Mahakama Kuu, Jaji Njoki Mwangi aliamua Bi Mueni alikuwa mwanachama wa Sacco na kuelekeza suala hilo katika mahakama ya kusuluhisha mizozo ya aina hiyo.

  • Tags

You can share this post!

DPP aamuru polisi kuchunguza video ya uchochezi

Jinsi Wajackoyah alivyojimaliza kisiasa ghafla

T L