• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 12:36 PM
Mwanamume akiri kuiba jozi ya viatu msikitini

Mwanamume akiri kuiba jozi ya viatu msikitini

NA RICHARD MUNGUTI

AFISA wa mauzo katika kampuni moja nchini anayedaiwa yuko na mazoea ya kuiba viatu katika msikiti ulioko katikati mwa jiji la Nairobi wa Jamia, ameshtakiwa kwa wizi wa jozi ya viatu vya thamani ya Sh10,000.

Musa Mohammed Jabir aliyefikishwa mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Milimani Lucas Onyina, alizua kioja alipodai angekufa njaa na angejisaidia kwa kuiba viatu.

Jabir aliyefunika mdomo wake baada ya kusomewa mashtaka, alizugumza kwa kigugumizi na kusema: “Wizi wa viatu ndio umenifikisha kortini. Wizi huu sio sawa ule mwingine wa mabavu.”

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda alieleza mahakama kuwa mshukiwa ameshtakiwa kwa wizi wa jozi ya viatu katika msikiti wa Jamia wakati wa ibada ya adhuhuri.

Upande wa mashtaka ulisema yuko na mazoea ya kutoweka na viatu katika msikiti huo wa Jamia.

Jabir alishtakiwa kwamba kati ya Mei 16 na Juni 9, 2023 aliiba viatu katika msikiti wa Jamia.

Mshtakiwa huyo alikamatwa Juni 12, 2023 na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Central kuhojiwa.

Jabir alishtakiwa aliiba jozi ya viatu mali ya Abdi Mohammed muundo wa Puma vya thamani ya Sh10,000.

Alipokanusha mashtaka hakimu alimuuliza: “Unafanya kazi?”

Jabir alijibu kwamba anafanya kazi jijini.

“Unafanyavkazi gani?” hakimu aliuliza.

“Kazi ya mauzo,” Jabir alijibu.

Hakimu aliendelea na kumuuliza mshtakiwa ikiwa anaishi Nairobi.

Mshtakiwa alijibu kwamba anaishi Nairobi kisha akaomba aachiliwe kwa dhamana.

Bw Gikunda (kiongozi wa mashtaka) hakupinga.

Hakimu alimwamuru mshtakiwa alipe dhamana ya Sh15,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa tena baada ya wiki mbili kutengewa siku ya kusikilizwa.

Mshtakiwa alipelekwa seli akisubiri watu wake wamlimpie dhamana.

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Miili 27 yafanyiwa upasuaji katika siku ya...

Rubis yawaweka sawa madereva Safari Rally ikianza

T L