• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Mzee ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la mabilioni Nairobi

Mzee ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la mabilioni Nairobi

Na RICHARD MUNGUTI

MZEE wa Kimasai ameshtakiwa kwa ulaghai wa shamba la Sh1.5 bilioni katika mtaa wa kifahari wa Karen, Nairobi.

Peter Leparakwo aliyewakilishwa na wakili Philip Nyachoti alikanusha mashtaka 20 aliyoshtakiwa pamoja na Fredrick Kimani.

Leparakwo na Kimani walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mahakama ya Milimani Lucas Onyina.

Akiwasilisha ombi la kuachiliwa kwa Leparakwo kwa dhamana, Bw Nyachoti alifichua kwamba “Wizara ya Ardhi inamtambua mteja wake (Leparakwo) kama mmiliki halisi wa shamba hilo.”

Bw Nyachoti alimpa Bw Onyina nakala ya barua kutoka kwa wizara ya ardhi iliyoandikwa mnamo Mei 30, 2022 ikimtambua Leparakwo kuwa mmiliki halisi wa shamba hilo.

Washtakiwaw amekana kulaghai shirika la bima la afya NHIF

Wakili huyo aliomba Leparakwo na Kimani waachiliwe kwa dhamana.

“Leparakwo ni mzee hawezi kutoroka. Shamba ni lake hahitaji kuling’ang’ania,” alisema Bw Nyachoti.

Hakimu aliwaachilia kwa dhamana ya Sh400, 000 pesa tasilimu kila mmoja.

Kesi itatajwa Mei 29, 2023 kwa maagizo zaidi.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Leo tunapika samaki ambapo tangawizi na...

Mshukiwa wa ujambazi ashtakiwa kwa kudai fidia ya Sh1.9...

T L