• Nairobi
 • Last Updated June 12th, 2024 4:24 PM
MAPISHI KIKWETU: Leo tunapika samaki ambapo tangawizi na krimu ya nazi ikiwa miongoni mwa viungo muhimu

MAPISHI KIKWETU: Leo tunapika samaki ambapo tangawizi na krimu ya nazi ikiwa miongoni mwa viungo muhimu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 2

Vinavyohitajika

 • samaki 2 aina ya Tilapia
 • vitunguu maji vyekundu 2 ambavyo unavikatakata
 • mashina ya giligilani ¼ kikombe; yakate vipande vipande
 • kijiko 1 cha tangawizi
 • punje 4 za vitunguu saumu; pondaponda
 • kijiko 1 cha maji ya limau
 • nyanya 2; katakata
 • kijiko 1 cha nyanya ya kopo
 • pilipili kijiko ¼
 • kijiko 1 cha poda ya kari (curry powder)
 • manjano kijiko ¼
 • gramu 250 za krimu ya nazi
 • majani ya giligilani kwa kupamba

Maelekezo

Kwenye kikaangio chako, mimina mafuta na chumvi na ongeza kwenye vitunguu maji vyekundu, mashina ya giligilani, tangawizi, vitunguu saumu, pilipili na maji ya limau. Pika hadi viwe laini na vyenye harufu nzuri.

Unaweza kuchagua kutotumia pilipili, au kuongeza zaidi au hata kidogo ikiwa unapenda. Ni kiungo cha hiari.

Subiri kwa muda kiasi hadi viive na viungo vyote vichanganyike pamoja. Katika hatua hii, mchuzi utakuwa mwekundu. Usiharakishe hatua hii kwani nyanya zinapaswa kuiva vizuri na viungo vinapaswa kuchanganyika vizuri.

Miminia krimu ya nazi na upike hadi mchuzi uwe mzito.

Ongeza majani ya giligilani kiasi na uyachanganye ndani. Chota mchuzi kiasi kwenye bakuli kisha ongeza samaki, na umwagilie sehemu ya mchuzi uliochota juu ya samaki. Acha samaki iive juu ya moto wa chini kwa dakika nyingine 10 hadi 15.

Hatua hii ni muhimu sana kwani inaruhusu ladha kujipenyeza ndani ya nyama na pia kuifanya iwe laini.

Mara tu ikiwa laini, pamba na majani mengine zaidi ya giligilani pamoja na limau iliyokatwa. Pakua na ufurahie.

 • Tags

You can share this post!

KUKABILI TATIZO: Uvimbe chini ya macho

Mzee ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la mabilioni Nairobi

T L