• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Nyuki wakatiza shughuli ya kusajili makurutu KDF

Nyuki wakatiza shughuli ya kusajili makurutu KDF

Na SAMMY WAWERU

ZOEZI la kusajili makurutu kujiunga na majeshi ya Kenya (KDF) katika kijiji cha Kinango, Kaunti ya Kwale Alhamisi lilisitishwa kwa muda baada ya bumba la nyuki kuzuka na kulivamia.

Kwenye video, vijana waliojitokeza wanaonekana kulala kwa tumbo ardhini, kundi la nyuki hao liliposambaratisha shughuli hiyo kwa kipindi cha muda usiojulikana.

Baadhi wanaonekana wakichana mbuga kukwepa kushambuliwa na wadudu hao hatari, huku maafisa kadha wa KDF waliokuwa wakisimamia zoezi hilo wakipiga doria kuzuia waliochujwa wasirejee tena.

“Ambia huyo mtu alale chini…toka nje…” mmoja akapaaza sauti. Kwenye video hiyo, baadhi ya watu wanaskika wakipiga nduru.

“Watu wa Kinango mko sawa kwa uchawi,” sauti nyingine ikaeleza kwa kejeli.

Katika video hiyo yenye urefu wa dakika mbili na sekunde mbili, maafisa wa KDF wanaskika wakihimiza vijana waliojitokeza kujaribu nafasi ya kazi kutulia nyuki hao wapite.

Zoezi kusajili makurutu kujiunga na kikosi cha jeshi linaendeshwa kote nchini. Lilianza mnamo Februari 8, 2021 na litaendelea hadi Februari 19, 2021.

  • Tags

You can share this post!

Akamatwa akijaribu kuhonga maafisa wa KDF

Hofu ya KSSSA kuhusu michezo ya Shule za Upili