• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 2:00 PM
Polisi sasa kuvaa sare mpya

Polisi sasa kuvaa sare mpya

NA WINNIE ONYANDO

POLISI sasa wataanza kuvaa sare mpya itakayochukua nafasi ya mavazi ya sasa ya bluu iliyokoleza ambayo wamekuwa wakivaa tangu mwaka wa 2018.

Miundo mbalimbali ya sare hiyo mpya kwa sasa iko South C jijini Nairobi ambapo maafisa na wananchi wanaalikwa kuitazama na kutoa maoni yao iwapo inafaa kupitishwa au kutupiliwa mbali.

Sare hiyo mpya ilizinduliwa kwa mara ya kwanza Februari 2023 wakati Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome alipoivaa wakati wa mkutano na naibu wake, Noor Gabow, Jaji Mkuu Martha Koome, na maafisa wengine katika Mahakama Kuu.

Serikali iliyopita ilifutilia mbali mavazi ya polisi ya rangi ya bluu ya aina kama ya sasa, ambayo yalikuwa yakitumika kwa miongo kadhaa.

Kwa sasa, maafisa wako huru kuvaa sare zote mbili hadi uamuzi wa mwisho utakapofanywa kuhusu sare mpya.

Wakati wa kampeni, Muungano wa Kenya Kwanza, ukiongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua, uliwaahidi maafisa kuwa utaondoa sare za polisi za bluu iliyokoleza.

“Mliteseka sana mikononi mwa (Fred) Matiang’i na (Karanja) Kibicho. Tutaondoa sare za sasa na kurejesha ya zamani,” Gachagua alisema wakati wa kampeni.

  • Tags

You can share this post!

Washukiwa wa wizi wa ng’ombe kuzuiliwa siku tatu...

USHOGA: Sheria tata yaanza kazi mshukiwa wa kwanza...

T L