• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Polisi watwaa daraja lililoibwa kutoka Mukuru-Kayaba

Polisi watwaa daraja lililoibwa kutoka Mukuru-Kayaba

Na SAMMY KIMATU

MAAFISA wa polisi walifanikiwa kupata vipande vya vyuma na mabati ya daraja moja lililokuwa limeporomoka baada ya kuibwa wiki jana.

Aidha, msako huo uliongozwa na mkuu wa tarafa ya South B, Bw Michael Were akishirikiana na kamanda wa polisi katika kituo cha polisi cha South B, Bw Samuel Ochoki.

Fauka ya hayo, Bw Were aliambia Taifa Leo kwamba kundi la washukiwa wanaohusishwa na uhalifu huo walifanikiwa kutoroka.

Isitoshe, aliongeza kwamba msako mkali wa maafisa wa polisi umeanzishwa ndiposa washukiwa wakamatwe.

Kando na hayo, alisema walifanikiwa kutwaa vyuma na mabati ya daraja linalounganisha mtaa wa mabanda wa Kayaba na mtaa wa mabanda wa Hazina.

Mitaa yote miwili iko katika kaunti ndogo ya Starehe.

Bali na hayo, Msaidizi huyo wa Kamishena wa kaunti aliongeza kwamba juhudi zao zao za kufanikiwa zilizaa matunda baada ya maafisa wa ujasusi kupashwa habari na wananchi kuhusiana na kisa hiki.

“Maafisa wa upelelezi walipashwa habari na wasamaria wema kuhusu tukio hili na mara moja tukachukua hatua ya kufika katika eneo vyuma hivyo vilikuwa vimefichwa kabla ya washukiwa kuviuza,’’ Bw Were akanena.

Kwa mujibu wa Bw Were, mali hiyo ambayo alifafanua kwa kina akiwaambia wananchi ili wajue ni mali ya serikali na kusema kwamba ilipatikana katika yadi moja ya vyuma kuukuu katika Eneo la Viwandani.

Kando na hayo, inakisiwa ya kwamba bei ya vyuma vyote na mabati yaliyotwaliwa ilikuwa yenye thamani isiyopungua Sh300,000 bei ambayo ni ya leo masokoni.

Baada ya kutwaa vilivyoibwa, mali hiyo ilipakiwa ndani ya lori la polisi na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Industrial Area ilikowekwa kama ushahidi.

Raia wasaidia maafisa wa polisi kubeba daraja eneo la Mukuru-Kayaba. Picha/ Sammy Kimatu

“Hii ni mali ya serikali iliyopatikana imeibwa ndiposa tunaitwaa na kuipeleka katika kituo cha polisi,’’ Bw Were akanena.

Vilevile, daraja lililoibwa lilikuwa llimejengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Rais wa Dondi za Jumuiya ya Madola Ulimwenguni (CWBC), Bw Reuben Ndolo.

Bw Ndolo alifadhili jumla ya daraja nne katika mitaa ya mabanda ya Mukuru kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Makadara zaidi ya miaka ya 20 iliyopita.

“Nimeelezwa historia ya daraja lililoibwa ilikuwa ni miongoni mwa zingine zilizojengwa chini ya ufadhili wa aliyekuwa wakati mmoja mbunge wa Makadara, Bw Reuben Ndolo.

Kando na daraja hili kuwahudumia wakazi kwenye mitaa ya mabanda kwenye maneo ya South B, iliwafaa kadhalika wafanyakazi na wafanyabiashara katika Eneo la Viwandani.

  • Tags

You can share this post!

Familia zaidi ya 100 zapoteza nyumba zao baada ya moto...

Phil Foden wa Man-City ndiye mwanasoka mwenye thamani ya...