• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Rais kuzindua Safari Rally ulinzi mkali ukiwekwa

Rais kuzindua Safari Rally ulinzi mkali ukiwekwa

RAIS Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzindua Mbio za Magari Duniani (WRC) Safari Rally nje ya Jumba la Mikutano la KICC mjini Nairobi hapo kesho.

Mbio hizo ambazo zitakuwa chini ya uangalizi mkali wa zaidi ya maafisa 1,000 wa usalama, zinarejea kwenye ratiba ya WRC tangu 2002.Zimevutia madereva 58 akiwemo bingwa mara saba wa dunia Sebastien Ogier.

Mfaransa huyu, ambaye anaongoza msimu huu utakaofika katikati wakati wa Safari Rally, yuko katika orodha ya madereva 24 wa kigeni.Hapo Jumanne, madereva walikuwa na shughuli nyingi ya kujifahamisha na barabara watakazotumia katika mashamba ya eneobunge la Naivasha ambako karibu mashindano yote yatafanyika.

Aidha, Kenya iliandaa mkutano wa Bara Afrika wa mbio za magari ulioendeshwa na rais wa Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA) Jean Todt hapo Jumanne. Waziri Amina Mohamed aliyehudhuria mkutano huo, alisema walisherehekea mafanikio ambayo yamepatikana katika Mbio za Magari za Afrika.

Aliongeza, “Rais Uhuru Kenyatta alisema mwaka 2019 wakati wa kuandaa mashindano ya kupima utayari wetu wa kurejeshwa kwenye WRC kuwa Safari Rally inaunganisha vyema moyo wa uwezekano. Kurejea kwa WRC nchini Kenya kutawapa watu wetu motisha ya kuendelea na maisha kwa umoja.

”Mapema Jumanne, Todt, ambaye aliwasili nchini Jumatatu akiandamana na msafara mkubwa wa maafisa kutoka FIA, alikutana na Wakurugenzi kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa Inger Andersen (UNEP), Maimunah Sharif (UN-Habitat) na Zainab Hawa (UNON) kuhusu mradi wa usalama na utoaji wa helmeti za bei nafuu.

Mjumbe huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usalama barabarani pia alikutana na maafisa kutoka Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA).

  • Tags

You can share this post!

Mwanahabari wa KBC aporwa

Ni Gor na Wazito huku nao Tusker wakitazama meza