• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 11:50 AM
Safari Rally kuwa na helikopta15, helipadi kuundwa

Safari Rally kuwa na helikopta15, helipadi kuundwa

Na AYUMBA AYODI

WAANDALIZI wa duru ya Mbio za Magari za Dunia (WRC) ya Safari Rally wataunda majukwaa zaidi ya ndege kusimama (helipadi) yatakayotumiwa na zaidi ya ndege 15 kwa mashindano hayo ya Juni 24-27.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Safari Rally, Phineas Kimathi alifichua Alhamisi kuwa hayo ni baadhi ya mabadiliko ambayo WRC imeomba kufuatia mafanikio ya duru ya Mbio za Magari za Afrika (ARC) ya Equator Rally iliyofanyika Aprili 23-25 katika maeneo ya Naivasha.

“Zikisalia chini ya siku 50 mbio za Safari Rally zifanyike, tunalainisha na kutekeleza mafunzo tuliyopata kutoka kwa Equator Rally,” alisema Kimathi.

Alikiri kuwa sehemu ya wanahabari kufanyia kazi yao pia itaaimarishwa kwa sababu, “ile iliyotumiwa wakati wa Equator Rally haikufikia viwango vilivyotakikana”. Mbio za Equator Rally zilikuwa na helipadi tano.

Kimathi alikuwa akizungumza wakati Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Nation Media Group (NMG) Stephen Gitagama alizuru afisi za Safari Rally katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Kasarani.

Gitagama alidokeza kuwa wako asilimia 90 tayari kuandaa duru hiyo.

Kimathi alisema anafurahia kukaribisha Gitagama na NMG kutafuta fursa za kufanya ushirikiano katika mbio nyingi za mashindano ya magari.

“Nafurahia kuwa NMG ina hamu ya kushirikiana na imefanya mazungumzo. Si kila siku unapata msafara mkubwa kama huu kutoka shirika kubwa,” alisema Kimathi.

Mbio za Equator Rally zilitumiwa kupima utayari wa Kenya kuandaa mashindano ya Safari Rally yatakayokuwa yakirejea kwenye kalenda ya dunia kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 19.

Magari kutoka kampuni za Hyundai, Toyota na M-Sport (Ford) yatashiriki mashindano hayo yatakayojumuisha kushindana katika umbali wa kilomita zaidi ya 797 katika kaunti za Nairobi, Nakuru na Kiambu.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Ghost Mulee akwama India baada ya Kenya kusimamisha safari...

Afueni kwa wakazi Githurai 45 barabara zikiendelea...