• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 11:00 AM
Seneta, wenzake wataka kuilipa kampuni iliyowashtaki Sh269 milioni

Seneta, wenzake wataka kuilipa kampuni iliyowashtaki Sh269 milioni

NA RICHARD MUNGUTI

KESI dhidi ya Seneta wa Trans-Nzoia Allan Chesang anayeshtakiwa kulaghai kampuni ya Makindu Motors Limited inayouza pikipiki za uchukuzi almaarufu bodaboda, jumla ya tarakilishi 2,800 za thamani ya Sh269 milioni akidai zinatakiwa na afisi ya aliyekuwa Naibu Rais (sasa Rais) William Ruto imechukua mkondo mpya.

Sasa Bw Chesang na washtakiwa wenzake Teddy Awiti, Kevin Matundura Nyongesa, Augustine Wambua Matata, Joy Wangari Kamau, James William Makokha almaarufu Wanyonyi na Johan Ochieng Osore wanataka kulipa kampuni hiyo ya MML inayomilikiwa na Musyoki Ngei pesa hizo.

Mawakili wanaomwakilisha Chesang na wenzake walimweleza hakimu mkuu mahakama ya Milimani Nairobi Bw Lucas Onyina “washtakiwa wanataka kulipia tarakilishi walizolaghai MML.”

Bw Onyina aliwaamuru wawasilishe ripoti jinsi watakavyolipa pesa hizo Septemba 21, 2021.

Pia Bw Onyina aliwaeleza washtakiwa ikiwa hawatakuwa na muafaka bora basi itabidi aendelee na kesi hadi tamati.

  • Tags

You can share this post!

Masaibu ya ndoa: Waigizaji Kate Actress na Phil Director...

Polisi waomba siku 14 kuwazuilia washukiwa 10 wanaohusishwa...

T L