• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 5:55 AM
Serikali yatwaa Sh102 milioni alizopokea mwanadada kutoka kwa mpenziwe mzungu

Serikali yatwaa Sh102 milioni alizopokea mwanadada kutoka kwa mpenziwe mzungu

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu imeruhusu serikali kutwaa Sh102 milioni ambazo raia wa Ubelgiji alimtumia mwanafunzi wa kike kama zawadi ya mapenzi.

Akisoma hukumu, Jaji Esther Maina mnamo Alhamisi amesema mahakama imeruhusu serikali idhibiti hela hizo zilizo kwenye akaunti mbili za benki zinazomilikiwa na mwanadada Felista Nyamathira Njoroge kwa sababu zinatokana na dili ya utakatishaji wa fedha.

Bi Nyamathira mwenye umri wa miaka 23 alipokea pesa hizo kama zawadi kutoka kwa bilionea Marc De Mesel.

Mahakama inasema chanzo bainifu cha hela hizo hakikutajwa licha ya Mesel kupewa muda ajieleze.

Ombi la kutwaa pesa hizo liliwasilishwa mahakamani na Shirika la Kutwaa Raslimali (ARA).

Stakabadhi zilizo kortini zinaonyesha alipokea hela kwa awamu nne kati ya Agosti 4 na Agosti 6 mwaka 2021.

Nyamathira alipata umaarufu mwaka 2021 alipodai kwamba Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilikuwa inazuia yeye kupokea takrima kutoka kwa mpenziwe.

Inadaiwa mwanamume huyo vile vile aliwatumia wanawake wengine watatu raia wa Kenya Sh257 milioni ambapo Tabby Wambuku Kago alipokea Sh108 milioni, Jane Wangui Kago (Sh49 milioni) na Serah Wambui (Sh100 milioni).

  • Tags

You can share this post!

Shakahola: Kindiki afungua rasmi awamu ya pili ya upasuaji...

Mhubiri ashtakiwa kwa ulaghai wa shamba la Sh60 milioni

T L