• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Tanzania yaambia raia waweke akiba nzuri ya mchele na mafuta sababu ya hali ngumu

Tanzania yaambia raia waweke akiba nzuri ya mchele na mafuta sababu ya hali ngumu

Na HAMIDA SHARIFF

Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Dkt Ashatu Kijaji amesema kupanda kwa bei ya mchele na mafuta ya alizeti mwezi Septemba, kunatokana na mahitaji ya bidhaa hizo kubwa makubwa hivyo amewataka Watanzania kuweka akiba ya chakula.

Dkt Kijaji anaamini kuwa akiba hiyo ya chakula itasaidia wananchi kuepuka kununua chakula hicho kwa bei ya juu katika siku za usoni.

Waziri huyo ameyasema hayo Ijumaa Septemba 15, 2023 jijini Morogoro wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu upatikanaji wa bidhaa, zikiwemo za vyakula na bei zake kama ilivyo kawaida ya wizara hiyo kutoa taarifa kila mwezi.

Alizitaka taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ikiwemo tume ya ushindani kufuatilia mwenendo wa bei za bidhaa zote kwa kulinganisha gharama za uzalishaji wa bidhaa hizo mkulima mzalishaji na mlaji.

“Ni kweli tupo kwenye soko huru lakini sio uhuru wa kumuumiza mwingine ndio maana mwaka jana mwezi Desemba, mlishuhudia kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi, lakini kutokana na hali hiyo, mliona Serikali tulivyochukua hatua na sasa tunaendelea na kazi yetu kwa kuhakikisha tunamlinda mzalishaji na mlaji,” akasema.

Katika hatua nyingine, Kijaji ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara kuepuka matapeli wanaotoa matangazo ya kuratibu misafara ya kibiashara nje ya nchi, akisema kuwa baadhi ya kampuni zinazotoa matangazo hayo zimekuwa zikiwahadaa.

“Hizi kampuni zimekuwa zikiwasajili wafanyabiashara na kuwataka watoe pesa kwa ajili ya kugharamia misafara hii, lakini nataka kuwaambia wafanyabiashara, kama wanataka kushiriki kwenye misafara hii ni vyema wakajiridhisha uhalali wa kampuni husika kutoka kwenye taasisi za Serikali ikiwemo Tan Trade,” akasema.

Hata hivyo, amesema kuwa tayari Serikali imeshaanza kufuatilia kampuni hizo na kuzichukulia hatua za kisheria.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adamu Malima, ameeleza namna mfumo wa stakabadhi ghalani ulivyowasaidia wakulima na hivyo kuondokana na uuzaji holela unaowanyonya wakulima.

Hata hivyo, Malima amesema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakipigana na mfumo wa kueleza maneno mengi na wengine ambao ni madalali wanajitahidi kukwamisha mfumo huo kutokana na maslahi yao binafsi.

“Hawa watu wanakwenda mpaka mashambani kwa wakulima kuwaambia Serikali hii mkipeleka mazao yenu kwenye maghala mtakaa wiki tatu bila kulipwa, pamoja na changamoto zote hizi lakini tunakuhakikishia sisi watu wa Morogoro tutakuwa wa kwanza kusimamia hilo,” akasema Malima.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi Waluo watakiwa ‘waache wivu’ kwa walioteuliwa...

Kenya kusafirisha shehena kubwa zaidi ya mbegu ya ng’ombe...

T L