• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Tanzia: Murang’a yapoteza mwanzilishi kampeni za sodo shuleni

Tanzia: Murang’a yapoteza mwanzilishi kampeni za sodo shuleni

Na MWANGI MUIRURI
SIMANZI imegubika Kaunti ya Murang’a kufuatia kifo cha mwalimu aliyezindua kampeni ya kwanza ya usambazaji wa taulo za hedhi – sodo katika shule miaka ya themanini (80’s).

Mwanaharakati huyo wa wasichana, Bi Angelica Magochi alifariki mwishoni mwa wiki iliyopita, na aatazikwa mnamo Ijumaa, Juni 30, 2023.

Kando na kuwa mtetezi kuimarisha ubora wa maisha ya watoto, Bi Magochi pia alikuwa akisisitiza walimu wawe wakipokezwa ushauri nasaha kuhusu afya ya kimawazo.

Alikuwa katika mstari wa mbele kushinikiza watoto wa kike mashinani wahamasishwe kuchukulia hedhi kama suala la kujivunia, wala sio la kuwatenga kijamii na kuwapa aibu.

Katika nukuu iliyochapishwa katika kituo cha redio cha

Kitaifa kwa lugha ya Gikuyu mnamo Aprili 26, 1985 Bi Magochi alisema kwamba “hapa mashinani suala la hedhi huwapa wasichana wa shule mahangaiko kiasi kwamba hukaa mbali na shule na wakijifungia kwenye nyumba”.

Aliongeza kwamba “kwa walio na wazazi wabunifu, huwa wanawapa wasichana hao vipande vya nguo kuukuu
au matambara ya magunia ili kujikinga na mahangaiko ya awamu hiyo ya kila mwezi kwa wanawake waliotinga umri”.

Alimalizia kwa kusema: “Ni dharura, wasichana hawa waonyeshwe kwa vitendo kwamba hedhi sio suala la aibu, ni la kawaida kiasi cha baraka na hilo tunaweza tu kuliafikia iwapo tutawapa uwezo wa sodo na kuwaonyesha jinsi ya kudumisha usafi”.

Kufuatia kampeni zake, wafanyabiashara Murang’a walizindua mradi kuwapa wasichana wa shule taulo hizo hadi wakati ilichukua jukumu hilo kuanzia miaka ya 2010.

Bi Wanjiku ni mamake Waziri wa Maji, Mazingira na usafi katika serikali ya Kaunti ya Murang’a Bi Mary Magochi.

Bi Magochi aliambia Taifa Leo Dijitali “mamangu alikuwa mpenda maendeleo ya kimaisha, mwenye itikadi kali kuhusu nidhamu, Muumini sugu wa kanisa la Kipresibeteria na aliyependa kutoa ushauri wa kimaisha”.

Alisema kwamba maneno yake ya mwisho kabla aage dunia yalikuwa ni “niko na amani moyoni, baraka zidumu katika jamii na taifa na maombi yangu haswa watoto wasajiliwe katika imani kwa Mungu na waafikie elimu bora bila gharama hasi”.

Mwendazake ambaye pia hivi majuzi alikuwa amempoteza bwanake Bw Magochi Munyu, alikuwa amestaafu majuzi na aliugua kwa muda mfupi kabla kufariki.

Amewaacha watoto wake watatu ambao ni Kamau Magochi, Waziri Magochi na Bw Njoroge Magochi.

Mwendazake atazikwa katika shamba lake lililoko Kijiji cha Mbogo-ini, wadi ya Kahumbu eneobunge la Kigumo.

Misa ya wafu itatangulia katika uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbogo-ini ambapo alifundisha kabla kustaafu.

[email protected]

 

 

 

  • Tags

You can share this post!

Mabadiliko ya tabianchi yalazimu wafugaji wa kuhamahama...

Warembo wa Gatura wajiimarisha kwa mchezo wa karate

T L