• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Warembo wa Gatura wajiimarisha kwa mchezo wa karate

Warembo wa Gatura wajiimarisha kwa mchezo wa karate

NA LAWRENCE ONGARO

HUKU mchezo wa karate ukizidi kuimarika eneo la Kati, kocha wa karate kutoka Murang’a Jediel Mutua amebuni timu ya karate ya warembo wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Gatura.

Kulingana na kocha huyo amekuwa na kikosi hicho cha wasichana 80 kwa muda wa miezi mitatu sasa.

Kocha huyo anasema lengo lake kuu ni kuwapa mazoezi makali ili kuelewa staili ya shotoka ikiambatanishwa na staili za kata na kumite.

Kwa sasa kocha huyo anawaandaa wanakarate hao kupandishwa gredi Julai 30, 2023 ili kupokea mshipi wa manjano.

Wakati huo pia anawatayarisha kwa mashindano ya karate ya shule za sekondari awamu ya tatu ya Mt Kenya Schools Karate League itakayoandaliwa katika chuo cha Kikatokiki cha Pastoral Centre mjini Thika mwezi Julai 22, 2023.

Alisema lengo kuu la kuwapa mazoezi ni kuwaweka kuwa na afya njema, kujikinga kutoka kwa adui, kuweka nidhamu, na kuzingatia utiifu kwa umma.

Alisema mwalimu mkuu wa Shule ya Wasichana ya Gatura Bi Agnes Gakuru amepongeza juhudi za kocha huyo kuzindua mchezo huo kwa wanafunzi wa kike.

Kocha huyo alisema mwalimu mkuu amekubali kununua sare za wanakarate hao ambazo ni changamoto wakati wa mazoezi.

Mutua anasema kuwa Chama cha Karate Nchini (KKF) eneo la Kati kimeweka mikakati kuona ya kwamba shule za upili eneo la Kati zinakumbatia mchezo wa karate.

Kulingana na mpangilio wa mazoezi ya warembo hao, ni siku ya Jumatano na Ijumaa kati ya saa kumi na saa kumi na moja na nusu za jioni.

  • Tags

You can share this post!

Tanzia: Murang’a yapoteza mwanzilishi kampeni za sodo...

Wito hazina ya kitaifa ya mashujaa ianzishwe

T L