• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 8:55 PM
Trump abebwa kama mhalifu wa kawaida baada ya kujisalimisha

Trump abebwa kama mhalifu wa kawaida baada ya kujisalimisha

NA XINHUA

TBILISI, GEORGIA

RAIS wa zamani wa Amerika, Donald Trump, aliachiliwa kwa dhamana Alhamisi baada ya kujisalimisha katika jela la Kaunti ya Fulton katika mji wa Atlanta, jimbo la Georgia.

Trump alijisalimisha kufuatia kesi yake ya kujaribu kubadili matokeo ya uchaguzi wa 2020, na uhalifu mwingine.

Alishtakiwa mapema mwezi huu kwa kukiuka sheria za jimbo la Georgia. Kadhalika, anakabiliwa na kesi zingine 13 katika majimbo tofauti ikiwemo Washington.

Kinyume na mara tatu ambapo amefunguliwa kesi katika miezi iliyopita, mara hii katika jimbo la Georgia alichukuliwa kama mhalifu wa kawaida kwa kupigwa picha na kunakiliwa kwa alama za vidole kwenye jela hilo.

Ni miongoni mwa matukio yaliyoibua hisia mseto katika taifa hilo tajiri na linalotetea demokrasia na mataifa mengine ulimwenguni huku wafuatiliaji wakigawika kuhusu kumuunga mkono kwa hadhi ya urais aliowahi kutumikia na kumkemea kwa kile anachodaiwa kuwa amehusika katika uhalifu katika taifa hilo.

Kando na kesi za kujaribu kubatilisha uchaguzi wa Rais Joe Biden, anatuhumiwa pia kujipatia nakala za siri za urais na kuzipeleka katika makazi yake ya kibinafsi ya Mar-A-Lago, jimbo la Florida wakati alipoondoka uongozini mapema 2021. Sheria za nchi hiyo zinazuia yeyote, akiwemo Rais, kujiwekea nakala za siri za kivita kama mali ya kibinafsi na kuhatarishwa kuonwa na walio na ruhusa haswa kama nakala hizo hazo hazijaachiliwa rasmi kuonwa na umma.

  • Tags

You can share this post!

Nitakupa kiti cha Kiongozi wa Upinzani ndio uache...

Raia wa Nigeria anayeshtakiwa kwa ‘washwash’...

T L