• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 8:50 AM
Tumeweka WiFi mpate kazi za kidijitali, serikali yaambia wakazi wa Kitui

Tumeweka WiFi mpate kazi za kidijitali, serikali yaambia wakazi wa Kitui

Na KANYALI BONIFACE

Waziri wa Mawasiliano na Habari Dkt Eliud Owalo amesema kuwa serikali kuu kupitia kwa wizara yake itaunganisha masoko 25,000 kwa mtandao wa intanet, hivyo kubuni nafasi zaidi ya milioni moja kwa vijana wasio na kazi nchini.

Waziri Owalo alisema haya Septemba 1, 2023 katika mji wa Mwingi, Kaunti ya Kitui alimokuwa akizidua mradi wa kuunganisha wakazi wa mji huo kwa mtandao wa WiFi, hii ikiwa ni baada ya kuzuru miji ya Kitui na Mutomo kuzidua mradi huo huo vile vile.

Akizungumza mjini Mwingi, Bw Owalo alisema kuwa kuunganisha vijana kwa mtandao ili waweze kufanya biashara lilikuwa suala kuu katika ajenda za Kenya Kwanza, hivyo serikali imo mbioni kutekeleza ahadi yake.

“Kwa kuunganisha vijana na mtandao, tunapania kutengeneza nafasi zaidi ya milioni moja za kazi,” alisema Bw Owalo.

Waziri huyo pia aliwarai Wakenya waunge mkono serikali ya Kenya Kwanza akisema kipindi cha siasa kimekamilika, na sasa kilikuwa kipindi cha kutekeleza ahadi za serikali kwa wananchi.

Bw Owalo pia alisema kwamba Wakenya hivi karibuni wataanza kujipatia simu za kidijitali (smartphones) kwa bei nafii ya Sh5,000 akisema uzinduzi wa simu hizo utafanyika kabla ya mwisho wa mwaka.

“Katika miezi miwili ijayo, serikali itazindua simu za bei nafuu ili kuwezesha wananchi kujipatia huduma za serikali pamoja na maudhui mengine ya manufaa haswa kwenye nyanja za biashara na elimu,” alisema.

Waziri wa Utalii na Wanyamapori Bi Penina Malonza aliyekuwa ameandamana na Bw Owalo kwenye hafla hiyo, aliwaomba wakazi wa Kitui kutilia maanani matumizi ya mtandao katika biashara na kujiinua kimasomo.

“Ni vyema vijana watumie mtandao vizuri ili kujiimarisha kibiashara ma haswa katika elimu,” alieleza Bi Malonza.

Naye Mbunge wa Mwingi ya Kati Dkt Gideon Mulyungi alishukuru serikali kuu kwa kutekeleza mradi huo mjini Mwingi, huku akiitaka serikali kuweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa mtandao hautumiki vibaya.

 

  • Tags

You can share this post!

Mwalimu afariki siku chache kabla ya kuanza kazi...

Pasipoti: Kindiki aendelea kuvunja makateli wa Nyayo House

T L