• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:54 PM
Wahalifu mtandaoni kuchukuliwa hatua – Matiang’i

Wahalifu mtandaoni kuchukuliwa hatua – Matiang’i

Na WINNIE ONYANDO

WALE watakaoeneza habari za uongo na zinazochochea chuki mtandaoni sasa wataadhibiwa vikali.

Hii ni baada ya serikali kuzindua Kamati ya Kitaifa ya Kupambana na uhalifu mtandaoni.Waziri wa Masuala ya Ndani, Fred Matiang’i akishirikiana na Waziri wa masuala ya Habari na Mawasiliano nchini, Joe Mucheru na Katibu katika Wizara ya Usalama na Masuala ya Ndani, Karanja Kibicho, jana Alhamisi walifanya uzinduzi huo katika Taasisi ya Kuboresha Mitaala ya Elimu ya KICD jijini Nairobi ili kupambana na uhalifu mtandaoni.

“Kwa miaka mingi, watu wamekuwa wakikandamizwa mtandaoni. Maneno ya uongo na ya kuchochea chuki yanasambazwa mtandaoni. Wahalifu wengi hawajapata kuchukuliwa hatua. Lakini baada ya uzinduzi huu, tutawakamata bila huruma,” akasema Dkt Matiang’i.

Kadhalika, alisema uzinduzi huo pia utawezesha ulinzi wa taarifa za kibinafsi za kampuni, kuwalinda watoto mtandaoni na nchi kwa jumla.

Kamati hiyo inajumuisha wasimamizi kutoka wizara ya masuala ya ndani, Mawasiliano, wapelelezi wa makosa ya jinai, vitengo mbalimbali vya maafisa wa polisi na mahakama kuu.

Aliitaka kamati hiyo itoe mafunzo kwa Tume ya Huduma za Mahakama kuhusiana na masuala ya mtandao na jinsi ya kuwaadhibu wahalifu hao.

“Mahakama ni sehemu muhimu sana katika mpango huu wa kupambana na wahalifu mtandaoni. Ikiwa watapata mafunzo kuhusu mtandao, wataweza kuwahukumu wahalifu bila huruma. Tumepokea ujumbe kuwa kuna mhalifu ambaye ameachiliwa kwa dhamana mara nane,” akasema Matiang’i.

You can share this post!

Naomba unikome!

MATHEKA: Wizara, idara za serikali ziige IEBC kutii mahakama

T L