• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
Wakenya kubaki bila kazi hoteli ya Hilton ikifungwa

Wakenya kubaki bila kazi hoteli ya Hilton ikifungwa

NA JURGEN NAMBEKA

IDADI kubwa ya Wakenya wanaohudumu katika hoteli ya kifahari ya Hilton katikati mwa jiji la Nairobi watapoteza kazi kufikia Desemba.

Hii ni baada ya kutangaza kuwa itafungwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya matatizo ya kifedha, yaliyotokana na kupungua kwa watalii wa kigeni baada ya janga la Covid-19.

“Kufuatia mazungumzo na wadau wote wa Hilton, shughuli zitasitishwa Desemba 31, 2022,” ilisema.

Kulingana na usimamizi wa hoteli hiyo, shida za kifedha zimechangia pakubwa kusimamishwa kwa operesheni ya hoteli hiyo ambayo serikali inamiliki asilimia 40.

Shida hizo zilitokana na kupungua kwa watalii kutoka nchi za kigeni, baada ya janga la Covid-19.

Hoteli hiyo ambayo iko katikati mwa jiji la Nairobi, imeeleza kuwa itafungwa licha ya kuwepo kwa zaidi ya miaka 50.

Usimamizi umeeleza kuwa, kuna sababu nyingine kando na Covid-19, zitakazofanya hoteli hiyo ifungwe.

“Covid-19 ilituathiri vibaya sana. Ila uamuzi wa kufunga Hilton hautokani tu na janga hili. Washikadau kadhaa wamekasirishwa na serikali kutowekeza pesa katika hoteli hii,” ilisema hoteli hiyo.

Licha ya hayo, hoteli hiyo imeeleza kuwa itajaribu kuhakikisha wafanyakazi watakaopoteza kazi, wamepata kazi kwingineko.

“Tutajaribu kuhakikisha wafanyikazi wetu hawaathiriki na kufungwa kwa hoteli yetu ya mjini. Wafanyakazi kadhaa tutawaajiri kwenye msururu wa hoteli zetu,” alisema msemaji wa Hilton.

Licha ya kufungwa kwa Hilton Nairobi, kampuni ya ‘International Hotels Kenya’ inayomiliki hoteli hiyo imeeleza kuwa itaendeleza operesheni zake katika hoteli zake nyingine.

Kampuni hiyo inamiliki hoteli za Hilton Hurlingham na Garden Inn.

  • Tags

You can share this post!

IMF yashangilia huku Wakenya wakiongezwa ushuru wa bidhaa

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Zakatul Fitr ni amri yake Mungu kwa...

T L