• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 7:50 AM
Wakili aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya ulaghai wa hisa

Wakili aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya ulaghai wa hisa

Na RICHARD MUNGUTI

HAKIMU mkuu mahakama ya Milimani alimwachilia kwa dhamana wakili anayeshtakiwa pamoja na wakurugenzi wawili kwa kula njama za kumlaghai mwenzao hisa ya kampuni.

Bw Victor Arara Were aliyekuwa Katibu wa Kilindini Warehouse (K) Limited (KWL) aliachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 na hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bw Lucas Onyina.

Akitupilia mbali ombi la upande wa mashtaka la kumnyima Arara dhamana, Bw Onyina alisema ni haki ya kila mshtakiwa kuachiliwa kwa dhamana isipokuwa ushahidi uwasilishwe kwamba “atawavuruga mashahidi ama atatoroka.”

“Hakuna ushahidi uliowasilishwa kuwezesha hii mahakama kumnyima mshtakiwa dhamana,” alidokeza Onyina.

Katika cheti cha mashtaka, Were anadaiwa alishirikiana na Awadh Swaleh Said na Swaleh Awadh Saleh kula njama za kumtimua Bw Omar Saleh Said katika kampuni ya Kilindini Warehouse (K) Limited (KWL).

Watatu hao wanadaiwa walitekeleza uhalifu miaka 24 iliyopita.

Hakimu alielezwa kuwa watatu hao Said, Saleh na Were walikula njama za kumwondoa Omari katika kampuni hiyo ya KWL kwa kubadilisha Fomu za hisa katika afisi za msajili wa kampuni.

Hakimu alielezwa na kiongozi wa mashtaka kwamba watatu hao waliokula njama hiyo baada ya Omari kutoa mtaji wake wa hisa katika kampuni hiyo ya KWL wa Sh39.9 milioni.

Hata hivyo Said na Saleh hawakufika kortini kama walivyoagizwa Aprili 4, 2023.

Kufuatia kutokafika kwao mahakamani kujibu shtaka Bw Anderson Gikunda aliomba mahakama itoe kibali cha kuwatia nguvuni.

Bw Onyina aliamuru polisi wawakamate na kuwafikisha kortini kujibu mashtaka.

Said, Saleh na Were wanadaiwa walikula njama za kumlaghai Omari miaka 23 iliyopita.

Were aliomba aachiliwe kwa dhamana lakini kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda akapinga akisema “watatu hao wamewasumbua polisi sana kuwafikia.”

Mahakama iliombwa ikatae ombi la Were kisha iamuru akae rumande hadi kesi itakapokamilika.

Were alishtakiwa alikula njama za kumlaghai Omari hisa katika KWL kati ya Desemba 1999 na Januari 2000.

  • Tags

You can share this post!

Mzozo wa shamba wamtia Mwanawe Meja Jenerali Mstaafu Joseph...

Mama amwiba binamuye Sh62, 000 kujilipa karo aliyomlipia...

T L