• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 10:50 AM
Mama amwiba binamuye Sh62, 000 kujilipa karo aliyomlipia shule

Mama amwiba binamuye Sh62, 000 kujilipa karo aliyomlipia shule

Na RICHARD MUNGUTI

MWANAMKE ameshtakiwa kwa kuiba Sh62, 000 na vyeti vya elimu vya binamuye akidai alikuwa anajilipa karo aliyomgharamia.

Esther Otete, 44 alishtakiwa kuiba cheti cha kuzaliwa, cheti cha KCPE, Cheti cha KCSE na Cheti cha Digirii kutoka Kisii vyake Bw George Momanyi.

Esther alikana kutekeleza uhalifu huo mnamo Oktoba 11, 2022.

Mbali na mashtaka ya wizi, pia alishtakiwa mbele ya hakimu mkazi Bw Eric Mutunga kwa kupatikana na mali aliyojua imeibwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

Esther alikana aliiba bidhaa hizo alipokuwa akiishi na Bw Momanyi katika mtaa wa Fedha eneo la Embakasi.

Mshtakiwa alipatikana na vyeti vya Bw Momanyi mnamo Aprili 30, 2023.

Esther adaiwa alikuwa akiishi na mlalamishi alipohepa na vyeti hivyo.

Aliishi na mlalamishi kwa wiki moja akiendelea na kupokea matibabu.

Mlalamishi alieleza polisi alichukua pesa hizo, Sh62, 000, mnamo Oktoba 10, 2022 kutoka kwa benki na kuweka ndani ya mfuko uliokuwa na vyeti vya kuhitimu shule za msingi, sekondari na chuo kikuu.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh80, 000 pesa tasilimu.

Kesi hiyo itasikizwa Septemba 5, 2023.

Bw Mutunga aliamuru kesi hiyo itajwe Juni 5 mshtakiwa aeleze ikiwa alikabidhiwa nakala za ushahidi.

  • Tags

You can share this post!

Wakili aachiliwa kwa dhamana katika kesi ya ulaghai wa hisa

Spika Wetang’ula aamuru walinzi wa wabunge...

T L