• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Wapishi ndani kwa wizi wa chakula cha shule

Wapishi ndani kwa wizi wa chakula cha shule

NA RICHARD MUNGUTI

WAPISHI wawili katika shule ya msingi ya Nairobi Primary waliokiri kuiba vyakula vilivyo na thamani ya Sh3,000 walitozwa faini ya Sh20,000 kila mmoja ama watumikie kifungo cha miezi sita gerezani.

Musyoka Kalola na Fred Nyakundi walikiri mbele ya Mwaniki Kamau kwamba walikamatwa kama wameiba na vyakula mbali mbali.

Baadhi ya vyakula walivyokuwa wameiba ni ndegu kilo mbili, pakiti mbili za unga, kilo mbili za sukari, kilo mbili za maharagwe, vitunguu saba, nyanya 23, chumvi kilo moja, nyanya na ndizi zilizokuwa zimeiva.

Wawili hao walikuwa wameziweka vyakula hivyo ndani ya magunia na masanduku.

Mshukiwa wa tatu hakufika kortini na mahakama iliamuru serikali itwae dhamana ya Sh5,000 aliyokuwa amepewa na polisi.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Munyao Mbondo alienda jikoni na kupata washtakiwa wamepakia vyakula hivyo ndani ya magunia.

Wapishi hao walishindwa kueleza chakula kilikuwa ‘kinafanya nini’ katika chumba chao cha kubadilishia nguo.

  • Tags

You can share this post!

Mang’u yang’aa katika mashindano ya somo la...

Ashtakiwa kwa kuiba taa ya gari katika kituo cha polisi

T L